Video:Alichosema Hashim Rungwe Mara Baada Ya Kuachiwa Kwa Dhamana
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam leo
September 6, 2017 limetoa ufafanuzi kuhusu ishu iliyokuwa inasambaa mitandaoni
kuwa aliyekuwa mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 na Mwenyekiti wa
CHAUMMA Hashim Rungwe amekamatwa.
Jeshi
hilo limesema kuwa kweli linamshikilia Hashim Rungwe ambaye alikamatwa tangu
August 28, 2017 akituhumiwa kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu.
Hashim
Rungwe anadaiwa kuhusika katika utapeli wa Dola za Kimarekani 30,800 ambazo ni
sawa na Tsh Milioni 73 kwa nyakati tofauti akiwa kama Wakili anayeendesha
biashara kati ya raia wa Uturuki Ally Riza Bilgen na Kampuni ya Les Tropiques
Group Mining SPRL Limited.
Inaelezwa
kuwa raia huyo wa Uturuki alikuja Tanzania kwa lengo la kununua korosho tani 15
na kuandikishana mkataba wa malipo ya Dola 72,000 kama gharama za bidhaa hiyo
na usafirishaji lakini tangu wamesainishana mkataba huo November 2016, hakuna
kilichofanyika na malipo hayo ya awali yalifanywa kwenye akaunti ya Rungwe
katika Bank ya CRDB.
Msikilize hapa hakitoa ufafanuzi zaidi==>>
No comments