Meya Wa Jiji La Dar Mhe Mwita Akutana Nakufanya Mazungumzo Na Meya Wa Jiji La Hin'an Nchini China
Mstahiki Meya wa jiji la Xn'an Nchini China Zhu Huan
akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mara baada ya
kufaya mazungumzo na mwenyeji wake Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya
Mwita alipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya
mbalimbali.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita
akisalimiana na Meya wa jiji la Xin'an Zhu Huan alipomtembelea ofisini kwale
leo na kufanya nae mazungumzo
Na Christina Mwagala, Ofisi Ya Meya Wa Jiji
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es
Salaam Isaya Mwita leo amekutana na kufanya mazungunzo na Meya wa Jiji la
Xin'an Nchni China Zhu Huan ofisini kwake Karimjeee.
Katika mazungumzo hayo , Meya
Mwita na mgeni wake wamejadili mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kukuza na
kutangaza utalii wa ndani na nje ya Dar es Salaam.
Aidha Meya Mwita amesema jiji
la Dar es Salaam lina kila aina ya vivutio vya utalii wa ndani na nje ambavyo
vinaweza kuwavutia wageni mbalimbali kutoka nje ya Nchi kufika jijini hapa na
kutalii badala ya kwenda Zanzibar , Kilimanjaro na maeneo mengine.
Ameongeza kuwa anaamini kuwa
mazungumzo hayo na mgeni wake yataleta tija na kwamba jiji la Dar es Salaam
litapata watalii kutoka sehemu mbalimbali na hivyo kuliwezesha jiji kupata
mapato makubwa kupitia vivutio vilivyopo.
“ Tunania ya kulitagaza jiji
letu kwenye sekta ya utalii, kutokana na rasilimali za vivutio vilivyopo,
ukienda kwenye maeneo mengi ndani ya jiji letu utaona kuwa tunavyo vivutio
vyakutosha kabisa ambavyo vikitangazwa kila mmoja atapenda kutalii katika jiji
hili” amesema Meya Mwita.
“ Yapo maeneo mengi ambayo
watanzania hawayajui, lakini kupitia mpango huu ambao nimekuja nao hivi sasa
ninaimani kwamba watu ambao walikuwa wanafika kwenye jiji letu na kupanda ndege
kwenda Zanziba ama Arusha na maeneo mengine, sasa watafanya utalii hapa kwetu”
amesisitiza.
Meya Mwita ametumia nafasi hiyo
kueleza kuwa , hivi karibuni jiji la Dar es Salaam linaratajia kupokea magari
ya utalii ambayo yamenunuliwa kupitia fedha za jiji, ambapo baada ya kufika
yatazinduliwa na hivyo kuanza kutangaza utalii wa ndani.
Kwaupande wake Meya wa jiji la
Xin’an Zhu Huan amempongeza Meya Mwit kutokana na uendeshaji wake wa jiji,
ambapo amesema jiji la Dar es Salaam limepata Meya bora ambaye anaamini kwamba
ataleta mabadiliko makubwa ndani jiji hili.
Mbali na pongezi hizo, pia
ameahidi kushirikiana nae katika sekta mbalimbali ikiwemo kutangaza utalii wa
jijini hapa ili uweze kutambulika katika maeneo mengine Nchini China.
No comments