Rungwe Aibuka Na Hili Kuhusu Bombardier
Mwenyekiti wa Chama cha Umma (Chaumma), Hashim Rungwe ameibuka na kumtetea Tundu Lissu kwa kile alichofanya kutoa taarifa juu ya ndege ya Tanzania kuwekwa kizuizini Canada na kusema ametumia haki yake ya kikatiba ya kutoa habari kuhusu sakata hilo.
Rungwe amezidi kuwashangaa watu ambao wanasema Tundu
Lissu siyo mzalendo kwa kuwa alitoa taarifa hiyo na kusema uzalendo siyo
kuficha au kufanya siri ya mambo yanayohusu maisha ya Watanzania na kudai
ni bora watu wajue ili mwisho wa siku hata maisha yanapokuwa magumu wajue kuwa
zile fedha za Umma zimechukuliwa kwenda kulipa deni hivyo watu wafunge
mkanda.
Aidha
Rungwe ameitaka serikali kufanya mazungumzo na watu hao japo waweze
kuwapunguzia au hata kama kulipa kwa awamu ili mwisho wa siku ndege hiyo iweze
kuja Tanzania na kuanza kufanya safari zake.
"Kesi ile imefikia katika hatua ya mwisho
kabisa ya utekelezaji, wanasheria wana mbinu nyingi wanaweza kufanya jambo wale
watu ambao ni wadai wakaelewa angalau kutupunguzia tukapata kanafuu fulani au
tukalipa hata kwa awamu ni nafuu ndege yetu ikaja ikaanza kufanya daladala yake
hapa na kupeleka watu hapa na pale kuokoteza hata hizo senti inaweza kujilipa
yenyewe ila ukitumia utemi utemi si kila kitu unaweza kutumia utemi" alisema
Rungwe.
No comments