Dc Mjema Ahaidi Kujenga Visima Viwili Kumaliza Tatizo Sugu La Maji Wakazi Wa Kata Ya Kiwalani.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Sophia
Mjema ameaidi kuwajengea visima viwili wakazi wa Kata ya Kiwalani ambavyo
vitasaidia kuondokana na tatizo sugu la maji linalowakabili.
Akizungumza na wananchi katika mkutano
wa wananchi na viongozi wa kata hiyo uliofanyika katika viwanja vya Shule
ya Msingi Yombo Kiwalani mara baada ya kushiriki zoezi la kufanya usafi katika
Chuo cha ufundi cha watu wenye Ulemavu.
Alisema maisha ya kila siku ya
mwanadamu anategemea maji katika kuendesha shughuli zake mbalimbali hivyo
atahakikisha anashirikiana na viongozi na wananchi wa kata hiyo kuhakikisha
wanamaliza changamoto ya upatikanaji wa maji katika kata hiyo.
Alisema wakati wananchi wa kata
hiyo wakisubiri mradi mpya wa Shirika la Majisafi na Majitaka (Dawasco) ili
iwatatulie tatizo la maji hivyo amewahakikishia atawajengea visima viwili
vya maji baada ya utaratibu kukamilka.
“Katika suala la maji nitahakikisha
wana wananchi mnapata maji safi na salama nyinyi na viongozi wenu mtapanga
kupanga maeneo ya kujenga “ Alisema Mhe Mjema.
Aidha akizungumzia kero ya usalama
katika kata hiyo kufatia kutokuwepo na kituo cha polisi amewataka viongozi
wa kata kuandaa eneo maalumu kwa ajili ya kujenga kituo cha Polisi yeye
kama mwenyekiti wa kamati ya ulizi na usalama atahakikisha anasimamia ujenzi wa
kituo hicho hili kuwasaidia wananchi kupata huduma wakati wowote.
“Vijana wengi wapo mitaani hawafanyi
kazi yeyote wanashinda usiku kucha katika mabar na vijiwe jambo ambalo linapelekea
vijana haonkujiingiza katika wimbi la kufanya vitendo vya uharifu” Alisema Mhe.
Mjema
Pia Mhe Mjema amewataka wamiliki wa
viwanda kuhakikisha wanaajiri wazawa ili kuepusha migogoro inayoendelea kwani
kwa kufanya hiyo kutasaidia kupunguza tatizo kubwa la ajila kwa vijana pamoja
na kupumguza wimbi kubwa la Vijana wanaokaa mitaani mpaka usiku wamanane bila shughili
maalum hivyo kuwa ndio chanzo kikubwa cha vijana wengi kujigiza katika matukio
ya uporaji.
Alisema kuna kazi nyingi za kufanya hasa
kwa vijana wazawa kama usafi na ulinzi hivyo wamiliki wa viwanda wanatakiwa
kuwaajiri wasiegemee kuwaajiri watu kutoka nje ya nchi.
Kwa upande wake MKuregenzi wa Manispaa
hiyo, Bw. Msongela Palela aliwataka viongozi wa Serikali za mitaa kujiepusha
vitendo vya rushwa pindi wananchi wanapohitaji huduma kama kusainiwa barua zao
za kujiunga na vikundi mbalimbali.
“Ukiona kiongozi yeyote wa serikali
anapokea hela kwa ajili ya kugonga muhuri usisite kuniletea taarifa ofisini
kwangu ili niweze kumchukulia hatua za kisheria” Aalisema Bw. Palela.
No comments