Kauli Ya Mhe Lowassa Kwa Rais Kenyatta Mara Baada Ya Mahakama Kufuta Matokeo Ya Urais Nchini Kenya.
Mjumbe wa kamati kuu ya (CHADEMA) na Waziri Mkuu
mstaafu Edward Lowassa amefunguka na kutoa pole kwa aliyekuwa Rais mteule wa
Kenya Uhuru Kenyatta kufutia mahakama ya juu nchini humo kufuta matokeo ya uchaguzi
wa Urais uliofanyika Agosti 8, 2017.
Mhe. Edward Lowassa anasema yeye bado
ataendelea kumuunga mkono Uhuru Kenyatta kwani ni kiongozi mwenye kusimamia
Demokrasia na mwenye maono ambaye anaweza kuisadia Kenya hivyo ataendelea
kumuunga mkono tena katika uchaguzi utaofanyika upya nchini humo.
"Nitumie nafasi hii kumpa pole Uhuru Kenyatta kwa jambo
lililotokea lakini nimpongeze kwa kufanya kampeni ya kiume kafanya kazi nzuri
sana, ukitazama maoni ya waangalizi mbalimbali walisema uchaguzi ulikuwa wa
huru na haki, lakini pia ukitazama orodha ya washindi wa wabunge Jubilee ndiye
inaongoza, kwa maseneta na magavana Jubilee ndiyo inaongoza picha hizi mbili
zinatoa picha, lakini ikishasema mahakama maamuzi yake ni lazima
yaheshimike"alisema
Lowassa.
Aidha Lowassa amesema kuwa anamuheshimu sana
Uhuru Kenyatta kutokana na jinsi ambavyo anaheshimu Demokrasia na kudai katika
kipindi cha uongozi chake siku zote amekuwa akilinda Demokrasia ya nchi hiyo
kwani wabunge wamekuwa na haki na vyama vimekuwa na haki na kila mtu ana haki.
"Niliwahi kumsikia mama mmoja akimtukana Uhuru Kenyatta matusi ya
nguoni kabisaa kiasi kwamba yule mama angekuwa hapa Tanzania siku nyingi
angekuwa jela lakini Uhuru Kenyatta alimsamehe na maisha yakaendelea lakini
uongozi wake ni uongozi wenye malengo amerithi nchi iliyotoka kwenye ugomvi wa
kivita lakini ameweza kuingoza kwa miaka mitano kimya wakifanya maendeleo, na
kwa maendeleo nadhani wametupita kwa sababu Uhuru Kenyatta kwa hiyo ni mtu
mwenye upeo, makini na mahiri ambaye anaitakia mema Afrika na Afrika
Mashariki" alisisitiza.
No comments