kufatia Kutolewa Nje Ya Darasa Na Mwalimu Kisa Damu Ya 'Hedhi' Msichana Ajiua.
Msichana wa umri wa miaka 12 ambaye ni
mwanafunzi wa shule ya msingi kusini mwa India amejiua baada ya mwalimu wake
kumuaibisha kwa sababu ya hedhi.
Katika ujumbe alioacha wakati
wa kujiua, alidai mwalimu wake "alimtesa".
Ingawa msichana huyo hakutaja
kisa hicho cha kuaibishwa kwa sababu ya hedhi, mamake msichana huyo anasema
aliagizwa na mwalimu wake kutoka nje ya darasa baada kwa sababu ya doa la damu
ya hedhi lililokuwa kwenye nguo zake.
Hedhi ni mwiko kuzungumziwa
hadharani India.
Wanawake kitamaduni huaminika
kuwa wachafu au hata waliolaaniwa wakati wanapopata hedhi.
Polisi wanasema wamepata
ripoti za kisa hicho cha kujiua na wanafanya uchunguzi.
Kisa hicho kilitokea Jumapili
katika wilaya ya Tirunelveli siku ya Jumapili katika jimbo la Tamil Nadu.
"Sijui ni kwa nini
mwalimu wangu analalamika kunihusu. Bado sielewi ni kwa nini ananihangaisha na
kunitesa hivi," mwanafunzi huo aliandika kwenye barua yake.
Alianza barua hiyo:
"Amma (mama), tafadhali nisamehe."
Mamake mwanafunzi huyo anadai
mwalimu huyo alimchapa binti yake siku za awali kwa kutofanya kazi yake ya
ziada.
"Binti yangu alipata
hedhi akiwa shuleni Jumamosi iliyopita," mamake ameambia BBC Tamil.
"Alipomjulisha mwalimu
wake, alipewa kitambaa cha kupangusa ubao atumie kama sodo.
"Mwalimu alimfanya binti
yangu kusimama nje ya darasa. Msichana wa miaka 12 atavumiliaje aibu ya aina
hiyo?" alishangaa.
Msichana huyo alijiua siku
moja baadaye.
Shule hiyo imeambia BBC
kwamba inashirikiana na polisi katika uchunguzi.
Chanzo-BBC
No comments