Breaking News

Kauli Ya IGP Sirro Kuhusu Ben Saanane


Jeshi la polisini nchini limesema bado linaendelea na upelelezi kuhusiana na kutoweka kwa Ben saanane ambaye ni msaidizi Wa mwenyekiti Taifa Wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA freeman mbowe.

Hayo yamesemwa mkuu wa jeshi la polisini nchini IGP simon sirro wakati akizungumza na katika kipindi na moja ya televisheni nchini ambapo amesema jeshi la polisi limeunda kikosi kazi Kwa ajili ya kulifuatilia suala hilo.

“Ndg mtangazaji jeshi la Polisi limeunda timu maalumu ya kufanya upelelezi ili kujua alipo Ben saanane kama yuko hai au raha hivyo wanaomba watu wenye taarifa kuhusu ben saanane kutoa taarifa Kwa jeshi la Polisi”.


Ben saanane alikuwa msaaidi wa mwenyekiti Taifa Wa chadena freeman mbowe na alipotea katika mazingira ya kutatanisha novemba 2016 hadi sasa hajulikani alipo.

No comments