Breaking News

Shaka Atutavumilia Watakaokiuka Taratibu Za Uchanguzi Kwa Kuanza Kampeni Mapema Au Vitendo Vya Rushwa.

Vijana 113 wa Jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) wamechukua fomu ya kugombea nafasi Uenyekiti taifa wa uvccm nafasi inayoshikiwa na mbunge wa dole Mhe Sadifa khamis Juma.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam Kaimu katibu mkuu wa UVCCM shaka hamidu shaka alisema jumla ya vijana 350 wa uvccm wamejitokeza kugombea nafasi mbalimbali ndani ya jumuiya hiyo.

Alisema UVCCM haito mvuumilia mtu au kikundi chochote kitakacho jihusisha na ukiukaji wa kanuni za uchaguzi ndani ya jumuiya hiyo ikiwemo kuanza kwa kampeni kabla ya muda wa uchaguzi kufika na kwamba wagombea wote watatangaza sera zao siku ya uchaguzi.

“Nitoe rai kwa Wagombea wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi  (UVCCM) kuacha kutumia lugha  chafu na dharau kwani tabia hizo zisipokemewa mapema zinaweza kukaribisha mvurugano, mgawanyiko na hatimae  kujipenyeza kwa adui rushwa” Alisema Shaka.

Aidha shaka ameiomba mamlaka ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (Takukuru) kufuatilia kwa karibu mienendo ya wagombea wa nafasi mbalimbali na wajumbe ndani ya jumuiya hiyo hili kuwabaini watakaojihusisha na vitendo vya rushwa.


Alisema kwa mujibu wa katiba ya jumuiya ya vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) inaonyesha kuwa Mwenzi Novemba mwaka huu umoja huo unatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi wake kwa ngazi mbalimbali za kitaifa.

No comments