Ziara Ya Mbunge Wa Temeke Mhe Abdallah Mtolea Kutembelea vikundi vya wajasiliamali jimboni kwake.
Mbunge wa Temeke Mhe.
Abdallah Mtolea akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ziara kutembelea
vikundi mbalimbali vya wajasilimali jimboni kwake.
Mhe.Mtolea akifafanua
jambo kwa Bi Magg Mum kutoka taasisi ya Global Fondation ya nchini uingereza katika ziara ya kutembelea
vikundi mbalimbali vya ujasiliamali jimboni kwake.
Mbunge wa temeke Mhe.
Abdallah Mtolea, pembeni yake ni Bi Magg Mum akisikiliza maelezo global Foundation ya nchini uingereza kutoka kwa
moja ya wasimamizi wa studio ya kurekodia maigizo (sinema) na mziki wa kizazi
kipya katika ziara hiyo.
Dar es salaam
Mbunge wa jimbo la
temeke Mhe. Abdallah Mtolea amefanya ziara ya kutembelea vikundi vya
wajasiliamali kukagua na kuona changamto wanazokutana nazo wakati wa kutekeleza
majukumu yao.
Akizungumza katika
ziara hiyo jijini Dar es salaam Mhe. Mtolea alisema lengo la ziara yake ni kujionea namna wajasiliamali
hao wanavyofanya shughuli zao pamoja na kusikiliza changamoto zao hili aweze
kuzitafutia ufumbuzi.
Alisema kwa kutambua ukosefu
wa mitaji pamoja na mazingira ya kufanyia kazi zao sambamba na teknolojia duni ni
moja ya vikwazo wanavyokutana navyo wajasiliamali hata mara baada ya kuwezeshwa.
Amezitaja changamoto
nyngine ni upatikanaji wa masoko ya
uhakika wa bidhaa wanazozizalisha pamoja na kutokuwepo na maeneo rasmi
ya kufanyia biashara zao.
Akizungumza mara baada ya kuwasili Mhe mtolea
katika kikundi chao msimamizi wa kituo cha Temeke Youth Hope saccos (Mwela Theater
Group) Bw.Hamadi Jongo aliesema anamshukuru Mhe mbunge kwa kuwawezesha kikundi
hicho kinachojishughulisha na kuuza mayai na kuku kuwa mkombozi kwa vijana.
Alisema kupitia kikundi hicho vijana wameweza
kujikwamua kiuchumi sambamba na kuwawezesha kuweza kufikia malengo yao kama
vijana.
Nao kikundi cha kinamama cha Tupambane na Umaskini Tuendelee
ambacho kilianzishwa kwa kushirikiana na ofisi ya mbunge kimekuwa na mafanikio
tangu kuanzishwa kwake 2016 kufatia kupatiwa mafunzo namna bora ya
kujiendelesha yaliyotolewa na kampuni ya Naimango Business Agency ya jijini Dar
es salaam.
Walisema kikundi hicho kinaendesha mradi wa kufuga
kuku wa kisasa ambao walianza na kuku 158 na kwa sasa wana jumla ya kuku 950.
Aidha Wamemwomba mhe mbunge kuwasaidia kupata eneo
waweze kukuza mradi wao kuku hili kujenga banda kubwa zaidi, kuanzisha mradi wa
kufuga samaki wa biashara pamoja na kulimba
mboga mboga na matunda.
No comments