Breaking News

Vijana tujenge mazoea ya kushiriki kazi za kujitolea kuliko kungoja kuajiliwa.

Katibu mkuu wa Asasi ya vijana ya Umoja wa mataifa inayojishulisha na maswala ya vijana (Yuna) Bw. Badru Rajabu amewataka vijana nchini kujenga mazoea ya kujitolea pasipokukaa nyumbani na kusubilia ajira.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani yaliyofanyika Katika Shule ya Sekondari Kibasila alisema kwa sasa imekuwepo dhana kwa baadhi ya vijana waliosoma kukaa nyumbani wakisubilia ajira kutoka Serikalini.

Alisema kitendo cha vijana hao kukaa nyumbani bila kuwa na kazi hata ya kujitolea au kujiajiri mwenyewe imekuwa ni vigumu kwao kuweza kupata ujuzi wa kufanyakazi.

“Kijana ukikaa nyumbani bila kujishughulisha kutafuta sehemu ya kufanya kazi hata ya kujitolea na elimu unayo kwa kungoja kazi kutoka serikalini au kuchagua kazi ni kumeshindwa kutumia elimu yako uiliyojifunza kutoka kwa walimu” Alisema Rajabu.

Alisema vijana anapoamua kuanza kujitolea kwenye taasisi mbalimbali za umma na za binafsi ni moja ya fursa ya kumwezesha kuapata ajira akiwa kazi ni pamoja na kuwasaidia vijana wengine ambao wanakosa ajira.
Kwa upande wake Msimamizi wa club za vijana kwa nchi za Afrika mashariki (EACYC) Bw.Samsoni Mwankemwa aliwoomba vijana kuweza kujiunga katika za vijana ili kuweza kuhamasishana namna ya kuboresha ongezeko la fursa za kazi kwa vijana watanzania pamoja na vijaa wenzao wa nchi za afrika mashariki.

Alisema kitendo cha kuwa na ongezeko la vijana katika taasisi za vijana kunaongeza uelewa na fursa za ajira kwa vijana ivyo kuweza kilisaidia taifa kuwa na maendeleo endelevu katika Nyanja ya uchumi.

“Unapokuwa na kikundi kikubwa cha vijana wanaoshirikiana katika kupeana ujuzi hasa katika mafuzo ya ujasiriamali kutasaidia kupunguza wimbi la vijana kukaa bila kazi” alisema Mwankemwa.

Aidha Bw. Mwankemwa ameiomba serikali iweze zaidi katika kuandaa mifumo mbalimbali ambayo itawasaidia kuongeza fursa za kazi kwa vijana kwa kuwawezasha kujiajiri ili waweze kujikwamua kiuchumi.

 “Ipo haya ya kuchukua hatua za makusudi kuboresha hali ya ajira za vijana wa kitanzania na vijana wanapata fursa ya kupata ajira zenye staha na zinazoendana na sheria na kanuni za kazi za kitaifa na kimataifa zilizopo” Alisema Mwankemwa.
 Moja ya kijana akiwashilisha mada katika maadhimisho hayo.
Washiriki wakisikiliza mada mbalimbali katika maadhimisho hayo.

No comments