Rais Magufuli Amteua Dkt. Abbas Kuwa Msemaji Mkuu Wa Serikali
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Hassan Abbas kuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari, Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.
Taarifa iliyotolewa na
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Hassan
Abbas umeanza tarehe 09 Agosti, 2017.
Kabla ya uteuzi huo, Dkt.
Hassan Abbas alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo na aliteuliwa
kushika nafasi hiyo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mujibu
wa Sheria ya Utumishi wa Umma namba 8 ya mwaka 2002.
Dkt. Hassan Abbas
ameteuliwa kushika nafasi hiyo kwa mujibu wa Sheria Mpya ya Huduma za Vyombo
vya Habari ya mwaka 2016, ambapo nafasi hiyo imebadilishwa kutoka Mkurugenzi wa
Idara ya Habari, Maelezo na kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari, Maelezo na
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mamlaka ya uteuzi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Gerson
Msigwa,
Mkurugenzi wa
Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar
es Salaam, 11 Agosti, 2017
No comments