Mhe Lema: Rais Akikosea Nitamsema Hadharani Siyo Chumbani, Sitaongea Uongo
Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema amefunguka na kusema kuwa wao kama viongozi
watamsifu Rais pale anapofanya vizuri hadharani na kusema anapokosea lakini
amedai hawawezi kumdhihaki Rais wala kusema mambo ya uongo dhidi yake.
Lema
alisema hayo jana katika mkutano wake wa tisa jimboni kwake kwenye Kata ya
Sekei Sanawari, Arusha Mjini na kusema anashangazwa na watu ambao wanasema Rais
hatakiwi kusemwa hadharani.
"Sitaongea uongo hadharani na sipo hapa
kumdhihaki Rais ila Rais akikosea nitamsema na sitamsema chumbani bali
nitamsema hadharani, habari ya nchi inavyoendeshwa tunasema hadharani, Rais
akikosea tutamsema hadharani na akipatia tutampongeza hadharani"
alisema Godbless Lema.
Aidha
Mbunge Lema aliendelea kutoa lawama zake kwa viongozi mbalimbali wa dini
akisema kuwa wamekuwa wakifumbia macho mbalimbali ambayo yanaendelea ndani ya
nchi hivyo ameahidi kuwa akimaliza mikutano yake atakuja kufanya mikutano
mingine kuhamasisha wanachi wasitoe sadaka kwa taasisi za dini kwa kuwa
viongozi hao wamekuwa wakifumbia macho na kushindwa kusema juu ya ukiukwaji wa
sheria ndani ya nchi na namna ambavyo Demokrasia imekupwa ikiminywa.
Mbali
na hilo Lema alisema anawashangaa watu wanaosema kuwa Mwanasheria wa CHADEMA
Tundu Lissu siyo mzalendo kwa kuwa ameweza kusema kuwa kuna ndege ya Tanzania
imeshikiliwa nchini Canada.
"Leo Lissu anakamatwa kwa sababu ya kusema
ndege ya Tanzania imekamatwa kwa kuwa tunadaiwa Ulaya, Polisi wanamchukua Lissu
na kwenda kumsachi kwake, mnatafuta ndege chumbani kwa mke wa Tundu Lissu,
wanasema Lissu si mzalendo sasa nani mzalendo aliyesema tunadaiwa Ulaya au
aliyetaka kuchukua fedha kinyemela akalipe deni Ulaya" alihoji
Godbless Lema
No comments