Meya Mwita Aishukia Nssf Malipo Bilioni 40 Ya Ujenzi Wa Machinga Complex
Meya wa Jiji Mhe Isaya Mwita
|
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam limemuomba waziri
nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa, Mhe George
Simbachawene pamoja na waziri wa fedha na mipango Dkt. Philip Mpango kuangalia
namna ya kutatua mgogoro uliopo kati halmashauri ya ya Jiji na mfuko wa hifadhi
ya jamii wa (NSSF) katika jengo la Dar es Salaam City Council Business
Park maarufu kama (Machinga Complex) kuafatia halmashauri ya jiji kutakiwa
kulipa deni la zaidi ya Bilioni 40 kinyume na mkataba.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo
Meya wa Jiji, Mhe Isaya Mwita alisema amefikia hatua ya kumtaka Waziri
Simbachawene kuingilia kazi mgogoro huo kutokana na kutorizika na hatua ya NSSF
kuwataka walipe bilioni 40 tofauti na mkataba unavyotaka walipe bilioni 12.45
.
Alisema halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ilingia mkataba wa ujenzi wa
jingo hilo na NSSF kwa mkopo wa shilingi bilioni 10 na mkataba huo ulifanyiwa
mapitio ambapo mkopo huo gharama ziliongezeka na kufanya mkopo kufikia shilingi
bilioni 12.45.
''Lakini makabidhiano ya jengo yalifanyika mwaka 2010 garama jengo
ilikuwa ni Bilioni 12.7 kwa sasa tunashangaa tunaambiwa na
hawa watu kuwaeti deni hilo linaladaliwa kuwa zaidi ya bilioni 40 sio bilioni
12.7 hatuwezi kukubali kabisa " Alisema Mhe Mwita.
Aidha Mhe Mwita aliongeza kuwa Halmashauri ya jiji imebaini kuwepo na ukiukwaji mkubwa wa kimkataba katika hatua za ujenzi wa jengo hilo kwakuwa mkataba unalitaka jengo hilo liwe na vizimba elfu kumi lakini badala yake limekuwa na vizimba elfu nne tu pamoja na gorofa ilitakiwa kuwa na gorofa tano upande mmoja na ghorofa sita upande mwingine lakini wamepewa jengo lenye gorofa nne kinyume na mkataba .
Alisema tangu
alipoingia madarakani uingoza Halmashauri ya jiji amekuwa akifanya jitihada za
makusudi kwa muda mrefu kutafuta muafaka na NSSF juu ya ulipaji deni hilo
bila mafanikio.
"Kwa
kutambua umuhimu wa urejeshaji wa fedha hizo ambazo zinazotokana na
michango ya wanachama wa mfuko huo na kwa kuzigatia hali halmahsauri ya
jiji tumebaini deni hilo halilipiki'' Alisema Mhe Mwita.
Pia Mhe Mwita aliongeza
kuwa jiji wako tayari kulikabidhi jengo hilo kwa NSSF ili wao waliendeshe
ili waweze kurejesha fedha zilizotolewa na mfuko huo kama
mkopo kwa halmashauri ya jiji kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo kutokana
na jiji hilo kushindwa kulipa deni hilo.
Alisema Mkataba
ulitaka NSSF kutoa fedha kwa Halmashauri ya Jiji kwa
ajili ya ujenzi wa jengo hilo jambo ambalo halikufanyika hivyo Halmashauri
hiyo haikuhusika na usimamizi wa fedha zilizokopwa na kuifanya
kushindwa kuthibitisha gharama zilizotumika .
No comments