Kauli Ya Rais Magufuli Kwa Mbunge Wa Cuf Tanga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amempiga biti Mbunge na viongozi wa
upinzani mkoani Tanga kutojisifia kuwa wao wameleta mradi wa Bomba la Mafuta
katika eneo la Chongoleani Tanga.
Rais Magufuli amesema kuwa
asitokee mtu yoyote katika jimbo hilo na kusema kuwa mradi huo wa bomba la
mafuta ameuleta kwani mradi huo umeletwa na serikali ya Magufuli chini ya Chama
Cha Mapinduzi.
"Hili bomba la mafuta
lingeweza kwenda kokote hapa Tanga, tungeweza kulipeleka hata katika majimbo
mengine ambayo yapo chini ya CCM lakini tumelileta hapa Chongoleani, sijui hata
chama gani kwa sababu serikali yangu haibagui chama inataka kuleta maendeleo ya
wananchi, hivyo tumeleta hili bomba la mafuta hapa ili kuleta maendeleo kwa
wananchi asitokee mtu yeyote akasema amelileta hili bomba, ashindwe na alegee,
limeletwa na serikali ya Magufuli" alisema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli na Rais wa
Uganda Museveni leo tarehe 5 Agosti 2017 wameweka jiwe la msingi la ujenzi wa
Bomba la Mafuta kutoka Hoima, Kaskazini mwa Uganda hadi Chongoleani Tanga.
Kata ya Chongoleani Tanga ipo
katika Halmashauri ya Tanga Mjini, jimbo ambalo lipo chini ya Mbunge Mussa
Mbaruk kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF).
No comments