Kauli Ya Kutaka Bangi Ihalalishwe Yamponza Mbunge Wa Chadema
Mbunge
wa jimbo la Tarime vijijini, kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) John Heche jana alikamatwa na polisi alipokwenda kituo cha polisi cha
Tarime kufuatilia kukamatwa kwa Katibu wake.
Mbunge
wa Jimbo la Serengeti Marwa Ryoba amesema kuwa polisi walimkamata Heche
kutokana na kauli zake ikiwepo kauli ya kutaka kilimo cha bangi kihalalishwe
pamoja na kauli yake ya kuzuia shughuli za ACACIA.
"Mhe.
Heche alifika Polisi Tarime kwa ajili ya kufuatilia kukamatwa kwa Katibu wake,
katika hali ya kushangaza naye akawekwa chini ya ulinzi na RCO na baadae
kuelezwa kuwa alikuwa akitafutwa kwa makosa mawili
"Kosa
la kwanza ni Kauli aliyoitoa mapema mwaka huu katika mkutano wa hadhara Sirari
ya kwamba atapeleka hoja bungeni aiombe serikali ihalalishe kilimo cha bangi na
pili kauli yake ya hivi karibuni kuhusu kuzuia shughuli za ACACIA Nyamongo
kufuatia Kauli ya Rais kwamba mgodi huo haupo kihalali nchini." alisema
Marwa Ryoba
Aidha
Mbunge Marwa anasema kuwa Heche alikataa kutoa maelezo yoyote polisi na jeshi
la polisi limechukua simu zake zote
"Walimwachia
Heche ila wakachukua simu zake zote na kumtaka afike polisi Jumatatu kwa
mahojiano. Alikataa kuchukuliwa maelezo yoyote kwa kuwa hakuwa amekwenda Polisi
kwa mambo hayo bali kushughulikia kukamatwa kwa Katibu wake, hivyo amejidhamini
na kuondoka ila simu zimebaki Polisi,
No comments