TCRA YAZIPIGA FAINI KAMPUNI ZA SIMU KWA KUTOFUATA TARATIBU ZA USAJILI WA LAINI
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) imezitoza faini kampuni zote za simu kwa kusajili laini bila
vitambulisho na kutofuata utaratibu.
Kampuni zilizotozwa faini hiyo na
kiwango kikiwa kwenye mabano ni Airtel (Sh1.08 bilioni), Smart (Sh1.3 bilioni),
Vodacom (Sh945 milioni), Zantel (Sh105 milioni) na Halotel (Sh1.6 bilioni).
Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James
Kilaba amesema leo (Julai 14) kuwa hii si mara ya kwanza kwa watoa huduma hao
kukiuka sheria.
Kiliba amesema kutokana na kurudia
kosa hilo, TCRA imeamua kuzitoza kampuni hizo faini hiyo.
Pia, kampuni hizo zimetozwa Sh500
milioni kila moja kwa kosa la kuathiri na kuhatarisha usalama wa umma na jamii
ya Watanzania kwa kusajili laini bila kufuata utaratibu.
No comments