MHE SUMAYE: HATUKO TAYARI KUZIBWA MIDOMO NA SERIKALI
Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani na
Mjumbe wa Halmashauri Kuu Chadema, Frederick Sumaye amesema kuwa licha ya
kukatazwa wasizungumze masuala ya kisiasa, lakini hawatanyamaza.
Akizungumza na vyombo vya habari leo,
Sumaye amesema kuwa wataendelea kufanya kazi kwa niaba ya wananchi ambao wana
imani nao.
Amesema nchi kwa sasa inakazana
kujenga mfumo wa demokrasia kandamizi ambayo kwa kiasi kikubwa inarudisha nyuma
maendeleo.
"Viongozi wa upinzani wamekuwa
wakikamatwa, wanawekwa rumande, wanatishwa lengo ni kudhoofisha upinzani,"
amesema Sumaye.
Amesema licha ya juhudi hizo za
kuwarubuni baadhi ya viongozi wakiwamo madiwani wachache, hawatadhoofika na
wataendelea kufanya Kazi.
Sumaye amesema kwamba wanataka
kujenga upinzani wa kweli wenye lengo la kusaidia wananchi.
Amesema katika kulihakikisha hilo
hadi kufikia mwaka 2018 hakutakuwa na kijiji, mtaa utakaokuwa hauna tawi la
Chadema.
No comments