Breaking News

WAZIRI JAFO - BODI YA WAKURUGENZI FCC ZIPATIENI UFUMBUZI CHANGAMOTO ZA UWEKEZAJI

Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Suleiman Jafo ameiagiza Bodi Mpya ya Wakurugenzi wa Tume ya Ushindani nchini (FCC) kukutana haraka kwa lengo la kupitia mambo yote yanayotakiwa kupatiwa ufumbuzi katika masuala ya uwekezaji Nchini.

Akizungumza Jijini Dar es salaam mara baada ya kuzindua bodi hiyo alisema bodi hiyo inajukumu kubwa la kumsaidia Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kufikia maono yake ya kuvitia wawekezaji na kukuza Uchumi wa Taifa.
"Kuna wakati mwingine makampuni ya nahitaji kuungana, lazima uwepo upembuzi (Analysis) haraka kuona je Muungano huo una tija kwa Taifa, kama una tija basi mfanye mchakato undelee kwa haraka,". Alisema Mhe. Jafo

Alisema FCC ni injini ya uwekezaji Nchini, nitoe Rai kwa bodi mpya kuiasaidia Wizara ya Viwanda na Biashara katika kuhakikisha Sekta Binafsi inakua kwa kasi na kuleta Maendeleo pamoja na kuondoa changamoto ya ajira kwa Vijana.
"Sekta binafsi ndio suluhisho la kujibu mahitaji ya ajira kwa Vijana husasani wanaohitimu kila Mwaka na jukumu hili tumepewa sisi Wizara ya Viwanda na Biashara,naomba sana FCC mfanye kazi yenu kwa uadilifu na uaminifu mkubwa". Alisema Mhe. Jafo

Aidha Waziri Jafo amewashauri watendaji wa FCC kutoa ushirikiano wa dhati kwa Bodi ya Wakurugenzi ili iweze kufanya kazi nakufikia malengo waliyojiwekea pamoja na kufanya kazi kwa kuzingatia mabadiliko ya sheria kwa kufanya tathmini ya namna makampuni yanavyoweza kuungana ili kuleta tija katika ushindani kibiashara.

Awali akizungumza wakati akimkaribisha waziri, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dokta. Hashil Abdallah amemshukuru Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa maono kutunga sera bora na kuweka mazingira rafiki jambo linalopelekea uwepo wa Mazingira ya tulivu ya ufanyaji Biashara Nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya (FCC), Dokta Aggrey Mlimuka amemhakikishia Waziri Jafo yeye pamoja na wajumbe wa bodi hiyo kutekeleza maelekezo yote aliyoyatoa kwa Bodi hiyo kwa ufanisi.

"Nichukue nafasi hii kwa niaba ya wenzangu nikuahidi kuwa tutafafanya maelekezo yote uliyotuelekeza kwa weledi Mkubwa kwa lengo la kumsaidia Rais Wetu kufikia maono yake ya kuhakikisha kuwa tuvutia wawekezaji na kuleta ushindani wenye usawa katika taifa letu". Alisema Dkt. Mlimuka.



No comments