WAZIRI KAIRUKI: ZAIDI YA NAFASI 10,184 ZIMETANGAZWA KUZIBA PENGO LA WALIOBAINIKA KUWA NA VYETI FEKI.
Serikali imetenga
zaidi ya shilingi bii 605 za nyongeza katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18 kwa
ajili ya watumishi waliopandishwa na wanaotarajiwa kupandishwa vyeo pamoja na
ongezeko la mshahara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala
bora Mhe.Angela Kairuki amesema
hayo jijini dare s salaam wakati akifungua semina elekezi kwa watumishi wa umma
waliopandishwa na kukabidhiwa barua za kupandishwa vyeo lakini zoezi hilo
likasitishiwa kutokana na zoezi la uhakiki wa vyeti.
Alisema fedha hizo pia zitalipa malimbikizo ya mishahara kwa watumishi
hao pamoja na kuwezesha kutekeleza zoezi zima la ajira mpya ambazo zimetangwa tayali
na serikali. “Tayari serikali imetoa kibali cha kuajiri
watumishi 10,184 kwaajili ya kuziba pengo la watumishi walioondolewa baada ya
kugundulika na vyeti feki” alisema Waziri kairuki.
Aidha waziri ametoa
agizo kwa wakuu wa taasisi zote za umma kuaajili wale ambao tayali
wameshahakikiwa ili kuepuka kuajili watumishi wasiokidhi vigezo vinavyotakiwa kama
wenye vyeti feki kufanya hivyo kutaathiri utendaji kazi.
No comments