Sheikh Ponda Alaani Waumini 10 Kutekwa Msikitini
Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu
Tanzania imelaani waumini 10 wa dini hiyo kutekwa wakiwa katika msikiti wa Ali
Mchumo wilayani Kilwa na sasa hawajulikani walipo.
Akizungumza leo Alhamisi Julai 27,
Katibu wa jumuiya hiyo, Sheikh Ponda Issa Ponda amesema Julai 21, mwaka
huu usiku waumini hao wakiwa wanasali katika msikiti huo walivamiwa na watu
waliokuwa kwenye magari matano.
Amesema wavamizi hao waliingia
msikitini na kuanza kuwapiga waumini hao kisha wakaondoka nao.
Amesema kabla ya kuingia msikitini,
walipiga risasi sehemu mbalimbali za msikiti huo.
Ponda amesema wakati wakitekeleza
unyama huo, majirani walisikia mayowe ya waumini hao.
Amesema baada ya hapo majirani
walishuhudia wavamizi hao wakiwa wamewabeba waumini hao na kuwaingiza kwenye
magari na kuondoka nao.
Amesema baada ya tukio hilo majirani
walishuhudia damu nyingi ndani ya msikiti huo.
"Sijui kama watu hao watakuwa
wazima hadi sasa kwa kuwa waliondoka wakiwa wamebebwa" amesema.
Amesema hadi sasa Polisi bado
hawajatoa taarifa zozote kuhusiana na waumini hao.
No comments