Lipumba Amvaa Maalim Seif, Asema Ndo Aliyewaponza Wabunge Waliotimuliwa
Mwenyekiti wa (CUF) anayetambuliwa na
ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa, Profesa Lipumba amefunguka na kusema kuwa
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad ana kesi ya kujibu na kudai
yeye kawaponza wabunge nane waliovuliwa uanachama wa CUF
Profesa Lipumba alisema hayo alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari na kusema Katibu Mkuu wa (CUF) Mhe.
Maalim Seif na yeye anayake ya kujibu mbele za Kamati ya Maadili na Nidhamu ya
CUF.
"Katibu
Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na kuna wananchama wengine wengi tu ambao pia wana
makosa ya kuweza kujibu mbele ya Kamati ya Nidhamu na Maadili katika watu wote
hao Katibu Mkuu yumo na yeye ndiye amewaponza hawa wabunge nane wa Viti Maalum
ambao wamevuliwa uanachama na ndugu zangu wa Zanzibar na wale wabunge wengine
wale msiwe mnasikiliza na kufuata kila anachosema Katibu Mkuu atakuponza kama
alivyowaponza wajumbe wa baraza la wawakilishi" alisema
Lipumba
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa CUF
Taifa Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema mpaka sasa wabunge wote nane
ambao wanasemakama wamefukuzwa uanachama wameamua kufungua kesi Mahakama Kuu
kupinga maamuzi feki ambayo yamefanywa na Baraza Kuu feki na kuitaka Mahakama
itamke kuwa wao ni wanachama halali wa CUF na wabunge halali wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Lakini pia Katibu Mkuu amesema kuwa
Baraza Kuu halali la CUF litakutana kwa dharura siku ya kesho Ijumaa tarehe
28/07/2017 kujadili mambo mbalimbali ambayo yanaendelea katika chama hicho na
kutangaza hatua ambazo zitafuata.
No comments