RAIS MAGUFULI AMUWEKA NJIA PANDA CHIZA
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi8ihd3N2rCgnpTzChxh2DtJXCVIaDFW8kGNffjK6suA0DqXWA-A72RU7_2TgPPeqaev87xsvSZGWI8ZMFoxIOfj2o8tVBDF8SCkitb8STdTHF79lsPP-wDAi1iv6jvXGiQexIHI580czdS/s640/Mhandisi+Chiza.jpg)
Rais John Magufuli ameshangazwa
na kauli ya Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo na
Biashara nchini Christopher Chiza kuwa na mipango ya kujenga majengo mapya kwa
ajili ya wafanyabiashara badala ya viwanda vitakasaidia nchi.
Akizungumza leo wakati wa ufunguzi wa
Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, Rais Magufuli amesema kwamba
ameshangazwa sana na mipangio ya kujenga mahoteli pamoja na kufanyia ukarabati
wa majengo kwani hajui mahali pesa hizo zitakapopatikana.
"Mh. Chiza amezungumza
kubadilisha majengo na kujenga mapya, mawazo mazuri lakini najiuliza hizo hela
zimetoka wapi , haingii akilini wao ndio wanatusisitizia mambo ya biashara na
viwanda na 'theme' ya mwaka huu inazungumzia kukuza biashara na maendeleo ya
viwanda sasa wao badala ya kuzungumza juu ya maendeleo ya viwanda wanataka
wajenge Hotel hapa, watengeneze majengo mapya sasa. Sijaelewa, sasa kama hizo
hela zipo basi mzipeleke mkajenge kiwanda cha mfano
Aidha Rais magufuli amesisitiza
kwamba "Haya majengo yaliyopo ambayo mnayaona yamechakaa hawa
wanaokuja kuonesha bidhaa zao wapeni bure wajenge ili kila mwaka wawe
wanaonesha, hiyo Hoteli kwani mkijenga lazima walale hapa hapa? Mnaweza kujenga
hoteli hapa bado wakaenda mjini. Mimi nilifikiri badala ya kujenga
jenga majengo fikirieni zaidi katika kujenga viwanda kwa ajili ya mfano wa
kuonesha Wizara kweli iko mbele kwa ujenzi wa viwanda.
Katika kuonyesha nia ya kufikia
Tanzania ya viwanda inafikiwa Rais ameitaka wizara pamoja na bodi hiyo
kutofikiria ujenzi wa majengo.
"Mwenyekiti nimekuteua juzi
umeshaanza kufikiria majengo hapa pamoja na Bodi yako mnanifanya nifikirie
zaidi. Haya majumba yanaweza yakawa siyo mazuri sana lakini ni mazuri kwa watu
wa Tanzania ambao wanataka kuona bidhaa. Yanayowaleta hapa siyo majumba Watanzania
wanakuja hapa kuangalia Teknolojia na vifaa vilivyomo.Inawezekana mimi nipo
tofauti mnisamahee lakini katika muelekeo wangu ninaona hizo hela mnataka
kuzitumia vibaya" Rais alisisitiza.
Pamoja na hayo Mh. Rais amewaomba
waandaji wa maonyesho hayo pamoja na Waziri wa viwanda na biashara Mh. Charles
Mwijage kuongeza siku zaidi katika maonesho ili watanzania waweze kupata
muda mzuri wa kununua na wafanyabiasha kuuza ambapo ombi lake lilikubaliwa hapo
hapo na kuongezwa siku tano mbele.
No comments