Rais Magufuli Amtumbua Kigogo Kwa Kuingiza Wasomali 50 Nchini
Rais
John Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi kwa naibu kamishna wa uhamiaji kwa
tuhuma za kuingiza nchini humo raia 50 wa Somalia na kuwapa vibali vya kuishi.
Kupitia
waziri mkuu Kassim Majaliwa kiongozi huyo ametaka kusimamishwa kazi mara moja
kwa bi Grace Hokororo na kuundwa kwa tume itakayochunguza utoaji wa vibali vya
uraia nchini humo.
Kauli
hiyo ilitolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumaliza kikao na
Makamishna wa uhamiaji kilichofanyika katika makao makuu ya uhamiaji jijini Dar
es salaam.
Tayari
Majaliwa amemuagiza waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba kubuni tume hiyo
ya uchunguzi.
Amesema
kuwa haiwezekani raia wa kigeni kuingizwa nchini humo na baadaye kupewa vibali
vya kuishi bila ya kufanyiwa uchunguzi wa kina.
"Idara
ya Uhamiaji tunaitegemea kusimamia mipaka yetu na kuziba mianya ya watu kuingia
bila ya kufuata taratibu lakini kwa mapenzi yake Ofisa huyu ameruhusu Wasomali
kuingia bila kufuata taratibu."
Waziri
Mkuu amesema ni lazima uchunguzi ufanyike ili kubaini ni kitu gani
kilichomsukuma kuwapatia vibali Wasomali hao ambao hawakuwepo nchini.
''Wameingia
na kupewa vibali moja kwa moja kwa mapenzi yake tu sasa hii ni dosari hatuwezi
kuivumilia."
Amesema
Serikali inaitegemea Idara ya Uhamiaji kwa kuzuia mianya ya uingiaji raia
mbalimbali kutoka nje ya nchi bila ya kufuata taratibu.
"Hawa
Wasomali aliowapa vibali vya kuishi wala hawakuwa wanaishi nchini wameingia tu
na kupewa vibali, hivyo Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli ameagiza ofisa huyo
akae pembeni na achunguzwe ili kujua ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa
raia hao."
Pia
majaliwa ameiagiza idara ya Uhamiaji kudhibiti kitengo cha utoaji hati za
kusafiria za Kibalozi na kwa wanaomaliza muda kutopewa tena.
"
Lazima hati hizo zikaguliwe katika mipaka yote na maeneo yote ya usafiri ili
kujua kama huyo anayeitumia bado anahadhi hiyo na msiporidhika ichukuweni kwani
kuna watu wanazitumia vibaya."
Hata
hivyo Waziri Mkuu ameagiza uchunguzi wa kina ufanyike kwa watu wote walioomba
hati za kusafiria pamoja na vibali vya makazi iwapo wanakidhi matakwa ya
kisheria kabla ya kuwakabidhi.
No comments