DC Hapi Amaliza Mgogoro Wa Ardhi Uliodumu Zaidia Ya Miaka 20
Wakazi waishio
Kunduchi kata ya Mtongani wametakiwa kuwa na amani kwakuwa serikali imesikia
kilio chao hivyo haitowaondoa katika makazi hayo na badala yake watapimiwa
maeneo yao rasmi.
Akizungumza jijini Dar es salaam na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally
Hapi katika mkutano na wakazi wa Kunduchi Mtongani kuhusu mgogoro wa
ardhi uliokuwa ukiwakabili kwa zaidi ya miaka 20 eneo ambalo awali lilikuwa
machimbo ya kokoto.
Mhe.Hapi
alisema amesikia mapendekezo ya manispaa na halmashauri ya Kinondoni na nmekubaliana
nayo hivyo kuwaeleza wakazi wanaoishi katika eneo hilo kuwa hakuna mtu
yeyote atakayekuja kuwaondoa makazi yao katika eneo hilo hivyo wawe na amani.
“Ameiagiza na
kuielekeza manispaa ya Kinondoni kuanza upimaji na kuhakikisha hati
zinapatikana mapema pamoja na kutenga maeneo muhimupindi wanapopima kama
barabara, hospitali, shule na polisi” alisema Mhe. Hapi.
Aidha Mhe Hapi amemuagiza Katibu tawala kuandika barua chuo kikuu cha
Ardhi ili kuomba wataalam kwenda kanza kufanya kazi ya upimaji katka eneo
hilo na kutoa wito watajadili kuona kama kutakuwepo na uwezekano wa wataalam
hao kuweza kuendesha zoezi la upimaji bila gharama zozote.
Amesema kuwa serikali
ya awamu ya tano chini ya
Rais Dk. JOHN POMBE MAGUFULI iko makini na
yenye kuwajali wananchi wake hivyo suala lolote linalohusu ardhi au kudhulumiwa
watoe taarifa kwakuwa serikali ipo tayari kupigania haki za wanyonge.
Kwa upande wake
mstahiki meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe.Benjamin Sitta amempongeza
Diwani wa kata kunduch Mhe. Maiko Urio kwa kazi nzuri na hatua ambazo amekuwa
akizichukua katika kuwaletea wananchi wa kata hiyo maendeleo hivyo kuwataka
wananchi kuwatumia viongozi wao kubainisha changamoto zao hili ziweze kupatiwa
ufumbuzi kwani maendeleo yanapatikana kwa kushirikiana na sio kwa itikadi Vyama.
Mapema akimkaribisha
stahiki meya wa kinondoni Diwani wa kata ya kunduchi Mhe. Maiko Urio alisema
kata hiyo imekuwa na changamoto nyingi lakini kutokana na ushirikiano anaopewa na
meya pamoja na mkuu wa wilaya ya kinondoni amekuwa akiweza kutatua chamgamoto
mbalimbali za wananchi kwa wakati.(Picha na Moshi Shabani)
No comments