RAIS MAGUFULI: ALIYEMUITA KAFULILA TUMBILI YEYE NDIYE TUMBILI…
Rais wa Jamuhuri wa Muungano Wa
Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amempongeza aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la
Kigoma Kusini, David Kafulila kutokana na namna alivyojitoa katika kutetea
maslahi ya Watanzania kwenye sakata la Escrow(IPTL) na kuonesha uzalendo mkubwa
ambao hawezi kusahaulika katika historia ya Tanzania.
Rais Magufuli ameyasema hayo
alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Nguruka katika hafla ya uzinduzi wa
mradi mkubwa wa maji uliopo Tarafa ya Nguruka katika Wilayani Uvinza ambapo
alisema kuwa akiondoka hapo bila kumpongeza Kafulila atakuwa amefanya dhambi ya
unafiki itakayompeleka motoni.
Akizungumza, Rais alisema anatambua
kwamba Kafulila yupo chama kingine, lakini kwenye suala la IPTL, aliweka
maslahi ya Taifa mbele na kusimamia ukweli hivyo anampongeza na pongezi hizo ni
za dhati kwani zinatoka moyo. Rais alieleza umma uliokuwa umejitokeza mahali
hapo kuwa, wizi uliokuwa unafanywa na IPTL ni mkubwa hivyo Kafulila alisimama
kutetea umma wa watannzani.
Lakini pia Rais alieleza vikazwo ambavyo
Kafuli alikutana navyo wakati akipambana kuhusu wizi huo uliokuwa ukiratibiwa
na baadhi ya watumishi wa serikali kwa manufaa yao wenyewe.
“Wakamtisha wengine kumpeleka
mahakamani, wakamtukana wee, wengine wakamuita tumbili, sasa tumbili amefanya
makubwa kwa ajili ya Watanzania. Wao ndio matumbili, huyu (Kafulila) alifanya
kazi ya Mungu ya kuwatumikia Watanzana,” alisema Rais Magufuli huku
wakazi wa eneo hilo wakilipuka kwa furaha.
Akiendelea kumwaga sifa hizo za
dhati, Rais Magufuli alisema kwenye hili suala la wizi wa IPTL, atampongeza
Kafulila kwa maisha yake yote.
Akizungumzia suala la uzalendo, Rais
amesema nchi ilikosa uzalendo na kwamba kila aliyekuwa akichaguliwa alikazana
kukusanya mali zake yeye mwenyewe bila kujua kuwa atakufa na atazikwa kwenye
shimo moja, hivyo akawasihi watanzania wajenge uzalendo.
Alisema maendeleo hayana chama na
kwamba, kiongozi mzuri ni yule anayewatumikia watu wake bila kujali chama,
kwani mradi huo wa maji anaoufungua utanufaisha watu wote hata wasio na chama.
Alieleza kwamba, ushabikia wa vyama ndio unaochelewesha maendeleo ya
watanzania.
Rais Magufuli amemaliza ziara yake ya
kikazi ya siku tatu Mkoani Kigoma kwa kuweka jiwe la msingi katika mradi wa
Maji mkubwa katika kata ya Nguruka uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni 2
ambao unatarajiwa kukamilika Disemba 30 mwaka huu ambao utafuta kero ya maji
kwa wananchi wa kata ya Nguruka.
No comments