Breaking News

PROF LIPUMBA AWAVUA UANACHAMA WABUNGE NANE WA VITI MAALUM PAMOJA NA MADIWANI WAWILI KWA KOSA LA KUKISALITI CHAMA

Baraza Kuu la Uongozi CUF chini ya mwenyekiti anaetambuliwa na msajili wa vyama vya siasa nchini Prof Ibrahim Lipumba leo limewavua uanachama Wabunge Nane wa Viti Maalum pamoja na Madiwani Wawili kwa kosa la kukisaliti chama.

Akizungumza makao makuu ya chama buguruni jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa chama Prof Ibrahim Lipumba alisema wabunge hao na madiwani waliitwa katika kamati ya nidhamu ya chama Jana kuhojiwa kutokana na kukiuka maadili ya uongozi hawakuweza kufika hata baada ya kupewa barua za kuitwa na kamati ya maadili hivyo baraza kuu limechukua maamuzi kwa kufuata katiba yake ya  mwaka 1984.

Alisema kwa mujubu wa tuhuma zilizotolewa na kamati ya maadili ni pamoja na viongozi hao kupewa maelekezo na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe  sambamba na kula njama ya kukihujumu chama ikiwemo kushiriki operesheni iliyoandaliwa na Chadema iliyoitwa (Ondoa Msaliti Buguruni), jambo linalokiuka katiba ya CUF.

Amewataja wabunge hao viti maalum na Madiwani waliovuliwa uanachama kuanzia leo 24/7/2017 ni Riziki Shahali Ngwali, Saverina Mwijage, Salma Mwassa, Saumu Sakala, Riziki Lulida, Mgeni Jadi kadika, Raisa Abdallah Mussa, Miza Bakari, Halima Ali Mohammed, Khadija Al Kassim, Leila Hussein Madibi (Diwani viti maalum ubungo) pamoja na Elizabeth Magwaja (Diwani viti maalum Temeke).

No comments