MHE MPINA: WACHUKULIENI HATUA KALI WANANCHI WATAKAOKAIDI KUTII MAAGIZO YA SERIKALI
Naibu waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe luhanga Mpina
akiongoza zoezi la kufanya usafi katika eneo la mchikichini manspaa ya
ilalajjni Dar es salam.
Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina Akisikiliza maelezo
kutoka kwa mkurugenzi wa kampuni ya usafi ya kejenjere trading Bw Mathew Andren
ambayo imekuwaikiendesha zoezi la usafi katika manispaa ya ilaa kata ya
mchikichini.
Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina amewataka viongozi Wilaya ya
Ilala kuwachukulia hatua kali watu wanaokaidi kutunza mazingira
yanayowazunguka.
kauli hiyo ameitoa jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akishiriki katika zoezi la usafi wa kila
mwisho wa mwezi.
Amesema kuwa ili kuweza
kuhakikisha zoezi hilo linatimia na kuwashirikisha wananchi wote, ni lazima
viongozi wawachukulie hatua kali wananchi ambao wanakaidi kushiriki
katika zoezi hilo kwani lipo kwaajili ya kuiokoa jamii na magonjwa
mbalimbali ya mlipuko.
“Ninyi viongozi mnatakiwa
kuwachukulia hatua kali wale wananchi wachache wanaokaidi kushiriki katika
usafi, kwani haiwezekani watu wailaumu Serikali kwa kila kitu, sisi viongozi wa
juu tuleteeni wale walioshindikana ili tuweze kuwashughulikia,”amesema Luhaga.
Aidha, katika hatua nyingine,
Luhaga amewataka wananchi kuunga mkono hatua za zinazochuliwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwani anania ya dhati
kuleta maendeleo ya nchi.
Hata hivyo, pamoja na hayo, Mpina
ameongeza kuwa katika awamu hii ya TanoTanzania imepata Rais wa kipekee ambaye
amekuwa mfano wa kuigwa barani Afrika na duniani kote.
No comments