ALICHOANDIKA MWANAMUZIKI TEKNO KWENYE MTANDAO KWA LUGHA YA KISWAHILI
Lugha ya kiswahili ni wazi inazidi
kuwa kubwa duniani kwa sehemu mbalimbali kuanza kuitumia na hata baadhi ya watu
maarufu kujaribu kuzungumza ili tu na wao wawe kwenye listi ya watu ambao
wanaweza kuzungumza kiswahili.
Star wa muziki kutoka
Nigeria, Tekno amekuwa mmoja wa watu hao ambapo kupitia akaunti yake ya
Instagram ameandika ujumbe kwa lugha ya kiswahili akielezea nyimbo yake mpya ya
Samantha kuwa inapatikana kwenye mtandao wa kuuza nyimbo wa Wasafi.
Tekno ameandika,“Wanasema
Utamu wa Ngoma uingie Ucheze….Haya watoto wazuri na wanangu wote wa Bongo Land
ardhi ya Nyerere, twendeni tukaonje Huu Utamu Wa Pini yangu mpya ya kuitwa
#SAMANTHA ila sio Mbwana….. ngoma iko Ndani Ya @wasafidotcom Kwa Mtonyo Wa Tsh
300 tu, Alafu Uje Unambie Umeionaje….Naskia eti Ngoma za Tekno hazijawai
kumuacha mtu Salama
.….Haya twendeni tukaliamshe
Dudeeeee!!!”
![😁](file:///C:\Users\Home\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.gif)
No comments