LHRC Yasikitika Wabunge wa CUF Kutumbuliwa Kukiwa Bado Kuna Kesi Mahakamani
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu,
(LHRC) kimetoa taarifa yake kwa vyombo vya habari kikisikitishwa na jinsi
Bunge, lilivyotengua uteuzi wa wabunge wa viti Maalum juzi.
“LHRC
inafuatilia mwenendo wa demokrasia nchini na kinatambua uwepo wa mzozo wa
kiutawala ndani ya CUF, mzozo ambao umepelekea mgawanyiko ndani ya chama hicho
na kufikia hatua ya wanachama kufikishana mahakamani kwa ajili ya usuluhishi,” imesema.
Taarifa hiyo iliyosainiwa na Kaimu
Mkurugenzi wa LHRC, Anna Henga imesema LHRC ilitaraji kuona Bunge likiheshimu
mhimili wa mahakama ambao bado haujatolea uamuzi shauri la Bodi ya Wadhamini ya
CUF dhidi ya maamuzi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ya kumtambua Profesa Lipumba
kama mwenyekiti.
“Kwa
maamuzi haya bunge limedharau mhimili wa mahakama ambacho ni chombo huru kwa
mujibu wa Katiba. LHRC kinalitaka Bunge kurejea maamuzi yake na kusitisha
maamuzi hayo mpaka mahakama itakapochukua hatua.” Imesema taarifa hiyo.
No comments