Mhe Masauni Awataka Wanafuzi Wanaosoma Masomo Ya Uhandisi Kuongeza Ubunifu Zaidi
Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani Mhe. Hamad Masauni ametoa wito kwa wanafuzi wanaosoma masomo ya uhandisi kuongeza
ubunifu zaidi ili kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa
viwanda.
Mhe. Hamad Masauni ametoa
wito huo wakati wa ufunguzi wa maonesho ya pili ya miradi mbalimbali
iliyofanywa na wanafuzi wa Chuo kikuu cha Mtakatifu Joseph, kilichopo
Mbezi jijini dare s salaam.
Alisema wanafuzi wanatakiwa
kuhakikisha wnawekeza katika swala la ubunifu ili nchi iweze kuwa na wabunifu
wakutosha hususani katika zama hizi za sayansi na teknolojia jambo ambalo litakuwa
chachu ya maendeleo.
“Katika Taifa lolote duniani
Serikali imekuwa inawategemea vijana wasomi katika fani mbalimbali
hususani uhandisi kuleta mapinduzi kiuchumi pamoja viwanda ili nchi iweze
kwenda iweze kusonga wabunifu wanahitajika .”alisema Masauni.
Alisema katika siku za
hivi karibuni kumekuwa na Shule nyingi ambazo zinafundisha kozi mbalimbali za
kihandisi tofauti na miaka ya zamani ambapo Vyuo vilikuwa vichache.
Serikali haitakuwa nyuma
kuwasaidia wanafunzi wabunifu wanatakao buni vitu mbalimbali ambavyo
vitalisaidia Taifa kuleta maendeleo ya haraka hususani katika
Viwanda.
“Nawaombeni wanafuzi kuwa
na imani na Serikali ya awamu ya tano ongezeni taaluma zaidi katika
masomo yenu vijana ndiyo nguvu kazi.” alisema Masauni.
Kwa uapnde wake Makamu
mkuu wa Chuo wachuo cha st Josoph, Bw. Bhaskara Raju alisema
wanafuzi hao wameweza kubuni mashine mbali mbali ikiwemo Gari lisilo tumia
mafuta pamoja na mashine ya kumenyea nazi ambapo zita wasaidia wanafunzi
wenyewe kujiajiri.
“Wakati serikali
inakwenda kasi kwa sera ya viwanda na wanafuzi wetu wamakuwa mstari wa mbele
kuweza kulitangaza taifa lwa kubuni vitu ambavyo vitaweza kuleta mabaliliko.”
alisema Raju
Aidha Bw. Raju aliongeza
kuwa maonesho hayo yamekuwa yakiwasaidia wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali
pamoja na wanafuzi wa sekondari kujifunza na kuona ubunifu unaofanywa wezao.
Naye Mmoja wa wanafuzi wa
Chuo hicho Meshack Zephania aliyetengeneza gari linalotumia umeme wa jua
alisema aliweza kuangalia mfumo wa gari ndipo naye akatengeneza.
“Mimi nilikuwa na mawazo
ya kutengezeza gari lakinio nilipo kaa na kuingia darasani kupatiwa mafunzo na
walimu niliweza kuunda kifaa hicho”. Alisema Zephania.
Pia aliwaomba wanafuzi wa
masomo uhandisi chini kuacha kukaa na mawazo yao kichwani bali
waweze kuyatendea kazi lilikukuza taifa kiuchumi
Kwa upande wake Bi Sophia
Abeld anayesoma chuoni hapo mwaka wa mwisho alisema Taifa likiwa na vijana
wanaokuwa na uwezo wakutengeneza vifaa mbalimbali za kiubunifu kama ya kupandia
mahindi wa watapunguza tatizo la ajira nchini.