Chama cha walemavu nchini
CHAWATA, kimeiomba serikali inayiongozwa na Rais John Pombe Magufuri
kuwapa nafasi stahiki pamoja na kuwapa nafasi katika fulsa zinazojitokeza ili
waweze kutumika katika ujenzi wa taifa na maendekeo ya taifa kwa ujumla.
Mwenyekiti wa chama cha
walemavu nchini (CHAWATA) Bw. John Mlabu alisema, jamii ya watu wenye ulemavu
wamekuwa wakipata shaka katika mipango wa nchi kuelekea kwenye uchumi wa kati sambamba
na sera ya tamzania ya viwanda.
"watu wenye ulemavu tunapata
shaka kushiriki katika mipango hii kwani tumekuwa tukiachwa nyuma watu wenye
ulemavu kila fuksazinazojitokeza kundi letu linabaki nyuma kwa muda mrefu hususani
katika nyanja za kielimu, uchumi, siasa, utamaduni na kijamii" alisema John Mlabu.
Hata hivyo chama hicho kimempongeza Rais John Magufuri kwa hatua ambazo
amet=kuwa hakichukua za kuzuia wizi wa asilimali za nchi pamoja na kuiweka nchi
katika uchumi wa kati na viwanda, pia kuwajali watu wa kipato cha chini
wakiwemo maskini katika taifa hili.
Aidha Bw.Mlabu wamemwomba Rais Magufuli kutokana
na usafiri wa bajaji kuwa maalum kwa matumizi ya walemavu wameiomba serikali
kuondoa kodi kwa vyombo ivyo pamoja na serikali kutoa kwa mkopo ya Bajaji kwa walemavu
kupitia umoja wao wa waendesha Bajaji mkoa wa Dar Es Salaam ambao watazitawanya
nchini kwa walengwa ambao ni wanachama wao.
|
No comments