Breaking News

BODI MASJID RIDHWAA KUJENGA CHUO CHA KISLAM NCHINI CHA AINA YAKE.

Bodi ya wadhamini ya Masjid Ridhwaa (RTMR) Mkwajuni ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kuanza ujenzi wa Chuo Kikuu cha Kiislam nchini kitakachowezesha wahitimu kujiajili na kuajiliwa.

Akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Bodi ya hiyo Bw. Alhaj Suleiman Seif Nassor alisema ujenzi huo wa ghorafa tano ambao unakadiliwa utagharimu shilingi bilioni 2.

Alisema ujenzi huo utakapo kamilika chuo hicho utakifanya chuo hicho kikuu waislam Tanzania (MUTA) kuwa moja ya chuo cha mfano kwa kuzalisha wahitimu ambao watakuwa wameandaliwa vizuri na kuwa na uwezo wa kujiajili pamoja na kutoa ajira kwa wengine mara baada ya kuhitimu.

Bw. Nassor alisema katika kuunga sera ya serikali ya awamu ya tano inayongozwa na Rais John Pombe Magufuli ya kujenga tanzania ya Viwada vya kati ndio jambo lilowasukuma kuamua kuanzisha chuo hicho ambacho kutaandaa wasomi ambao pindi watakapo hitimu masomo yao wataweza kujiajili na sio kungoja kuajiliwa.

“Azma kubwa ya kuanzishwa chuo hicho ni kuendeleza vijana kitaaluma na kisayansi kwa kuzingatia sera ya serikali ya awamu ya tano ya kujenga Tanzania ya viwanda vya kati” Alisema Bw. Nassor.

Tumepania kutoa mchango kwa kuitikia wito wa Rais Magufuli wa kuanzisha  viwanda vya kati kwa kuweka wasomi wenye mwelekeo wa kidigitali kwa mafunzo na vitendo zaidi ili kuondoa ugonjwa sugu kwa wahitimu kutafuta kazi.

Aidha bodi hiyo imetoa pongezi Rais Dkt.John Pombe Magufuri kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi cha miaka 2 tangu kuingia madarakani kwa hatua anazochukua kuziba mihanya ya wizi na ubadhilifu wa asilimali za nchi.

"Tumefurahishwa sana kwa Rais Magufuli kwa namna alivyofanikiwa kuinyoosha nchi, sambamba na kuwaokoa vijana wengi ambao walikuwa wamejiingiza katika biashara ya madawa ya kulevya”. Alisema  Nassor.

Alisema Bodi hiyo tayali ameshaiomba serikali ya Rais Magufuli kubaini na kubadili muundo wa shahada uliopo kwa sasa kwani unawaandaa wahitimu kutafuta ajira serikalini na kwenye makampuni binafsi badala yake kuandaa masomo yatakayo waandaa kujiajili tangu wakiwa katika mwaka wa pili wa masomo ya kidigitali.


Pia alibainisha kuwa (MUTA) imejipanga kuajili walimu wasiopungua 42, sambamba na kujenga misikiti, vituo vya elimu, vituo vya afya na kufanya miradi ya uchumi kwa kuzingatia misingi ya kiislam pamoja na kufanya mambo yote ya maendeleo.

No comments