Breaking News

KADA WA CCM KUZINDUA KAMPENI YA “MAGUFULI BAKI” NCHI NZIMA.

Aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Sengerema kura za maoni CCM 2015,Bw.Laurence Mabawa akifafanua jambo katika mkutano wake na waandishi wa habari mapema leo jijini dar es salaam, kushoto kwake ni Bi. Georgina Misana Afisa habari Idara ya Habari malezo

Dar es salaam
Watanzania wametakiwa kumwunga mkono jitihada zinazofanywa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa na nzuri anayoendelea kuifanya ya kutetea na kupigania rasilimali za taifa.

Wito huo umetolewa Jijini dar es salaam na aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Sengerema kura za maoni CCM 2015, Bw. Laurence Mabawa alisema ni vyema watanzania wote bila kujali jinsia, dini wala makabila kumpongeza na mkumtia moyo Rais na serikali yake na sio kumkatisha tamaa.

Alisema pamoja na jitihada zote anazoendelea kuzifanya Rais Magufuli wapo baadhi ya wanasiasa na kikundi cha watu kimeibuka na kuanza kutoa lugha za mahudhi na kejeli kuhusu jitahada hizo sambamba na kwa wananchi wanaojitokeza hadharani kumpongeza rais na serikali yake.

Kundi hilo limekuwa likiendesha propaganda katika mitandao ya kijamii na kupitia vyombo vya habari kuwa watu wanaojitokeza hadharani kuwa wanajipendekeza jambo ambalo si la kweli kwani kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muunganowa tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 18 inatoa nafasi kwa kila mtanzania kutoa maoni yake.

Aidha Bw. Mabawa aliongeza kuwa kwa kutambua na kuthamini mchango wa Mhe rais ameamua kuanzisha kampeni ya “MAGUFULI BAKI’ ambayo itahusisha mikoa yote ya tanzania bara kwa kuwafikia wanafunzi wa sekondari na wananchi kumwunga mkono Rais Magufuli kuendelea kusimamia msimamo wake wa kuwatetea watanzania wanyonge na maskini.

Alisema kupitia kampeni hiyo ambayo itaendeshwa kupitia mitandao ya kijamii maalum pamoja na vyombo vya habari itawapa fursa wananchi kutoa maoni yao kuhusu utendaji wa Rais Magufuli na serikali ya awamu ya tano kwa ujumla ikiwa ni kupongeza au hata kukosea.

No comments