MAUZO YA HISA DSE YAMESHUKA KWA ASILIMIA 36 WIKI HII.
Mauzo
ya Hisa (Turnover/ Liquidity)
Thamani ya mauzo
ya hisa kwa wiki hii imepungua kwa 36% kutoka Shilingi bilioni 6 wiki
iliyopita hadi Shilingi bilioni 3.9 wiki hii iliyoishia tarehe 14 Julai 2017.
Hata hivyo idadi ya
hisa zilizouzwa na kununuliwa imepanda kwa 26% kutoka hisa 13.6 wiki iliyoisha
tarehe 6 Juni 2017, hadi hisa milioni 17 kwa wiki iliyoishia 14 Julai 2017.
Kampuni
zilizoongoza katika mauzo ya hisa ni kama ifuatavyo:
CRDB -89%, TBL -8%, DSE
-0.9%
Ukubwa
Mtaji (Market Capitalization)
Ukubwa wa mtaji wa
kampuni zilizoorodheshwa katika soko umepanda kwa Shilingi Bilioni 516 kutoka
Shilingi Trilioni 18.7 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 19.2 wiki
iliyoishia tarehe 14 Julai 2017. Hii ni kutokana na kupanda kwa bei za hisa za
USL (34%), ACA (9%) na JHL (5%).
Ukubwa wa mtaji wa
kampuni za ndani umepanda kwa Shilingi Bilioni 13.5 kutoka Shilingi Trilioni
7.70 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 7.72 wiki hii. Hii ni kutokana na
kupanda kwa bei ya hisa za CRDB (2.5%).
Hati
Fungani (Bonds)
Tofauti na ilivyokuwa
kwenye hisa, mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia tarehe 14 Julai 2017
yamepanda kutoka Shilingi bilioni 12.25 wiki iliyopita hadi Shilingi Bilioni
44.3.
Mauzo haya yalitokana
na hatifungani kumi na saba (17) za serikali na za Makampuni binafsi (Corporate
Bonds) zenye jumla ya thamani ya Shilingi bilioni 51 kwa jumla ya gharama ya
Shilingi Bilioni 44.3.
Viashiria
(Indices)
Kiashiria cha kampuni
zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepanda kwa pointi 59 kutoka pointi
2,151 hadi pointi 2,211 kutokana na kuongezeka kwa bei za hisa za kampuni mbali
mbali zilizopo sokoni.
Kufuatia kupanda kwa
bei za hisa, kishiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimepanda kwa pointi 6
kutoka pointi 3,666 wiki iliyopita hadi pointi 3673 wiki hii.
Kiashiria cha sekta
ya viwanda (IA) imebaki kama awali kwenye wastani wa TZS 4809.
Kiasharia cha huduma
za kibenki na kifedha (BI) wiki hii kimepanda kwa pointi 17 kutoka pointi 2,598
hadi pointi 2,616 kutokana na ongezeko la bei ya hisa za CRDB (2.5%).
Kiashiria cha Sekta
ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imebaki kwenye wastani wa 2,467 kama awali.
Shindano
la Wanafunzi la Uwekezaji
Shindano la DSE SCHOLAR INVESTMENT CHALLENGE 2017
lilifika mwisho tarehe 30 Juni 2017. Zaidi ya wanafunzi wa vyuo na secondary
12,000 walishiriki katika shindano la mwaka huu, ikiwa ni Zaidi ya mara 3 ya
mwaka uliopita, 2016.
Matokea ya washindi
wa shindano hili yatatangazwa tarehe 18 July 2017 baada ya kufanyika tukio la
mwisho la kuhusisha wanafunzi 10 bora kushiriki katika kipindi cha maswali na
majibu na washindi watatu (3) kuamuliwa
na jopo ya majaji wa shindano hili.
No comments