SPIKA NDUGAI AFUNGUKA, BAADA YA WABUNGE WA UPINZANI KUSUSA FUTARI ALIYOANDAA DODOMA
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhPG6AqUZgP0Nxx0Sze23JmN1EN7QgkJizSRB2kOawBDLd91SLgw-cwEdBSdAbQTu6DuXAIC1PC2aeZc1_tKADJeW4E6AxeWSlpT1mIYP6EUBqPOJNMv0_aHotJfi5mbq99bgJGgAmhyLUv/s640/1.jpg)
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Job Ndugai amewakumbusha wabunge wa vyama vya upinzani hasa vinavyounda UKAWA umuhimu wa jamii kukaa pamoja, kujadiliana na kumaliza tofauti zao.
Ndugai ambaye ni mmoja wa wabunge wa
Bunge la 11 aliyasema hayo baada ya baadhi ya wabunge hasa wa upinzani kususia
futari aliyoiandaa siku ya Jumanne kwa ajili ya wabunge wote. Kiongozi huyo wa
juu wa mhimili huo alisema kuwa licha ya jukumu zito la kujadili na kupitish
bajeti ya serikali ya 2017/2018, ushirikiano kwa jamii ni muhimu.
Jambo hilo lilmfanya asiwe na raha na
kuamua kuzungumzia ndani ya bunge kwa upole kabisa ambapo alisema kuwa, baada
ya kuhudhuria futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu Jumatatu, na baada ya kuwepo
tetesi za kususia ya kwake alisema, amejifunza kuwa baadhi wamekatazana
kuhudhuria shughuli kama hizo.
“Lakini nikajifunza kitu kimoja
ambacho sikupenda kukisema, ila nikiseme hapa kidogo. Kuna wenzetu wamekatazana
rasmi kuhudhuria shughuli kama hizi.”
Ndugai aliyasema hayo Jumanne wakati
akihitimisha kipindi cha maswali na majibu kabla ya kupisha mapumziko na kisha
kupigiwa kura kwa bajeti ya serikali.
"Bunge linaendeshwa kwa
mawasiliano ya namna mbalimbali baina ya wabunge na uongozi. Endapo kuna jambo
linakwaza na kusababisha watu wasipate futari pamoja, ni vizuri wakae pamoja na
kuondoa jambo hilo," alizungumza Ndugai.
Licha ya kutoa tahadhari hiyo, Ndugai
alisema kuwa wabunge hao wana uhuru wa kufanya hivyo (kutohudhuria) kama
wanaona ni sawasawa.
“Siyo mwezi wa chuki na kubaguana.
Niwakaribishe tena kwenye futari kwa watakaoweza kufika. Watakaoshindwa In Sha
Allah, kila la heri. Tutaendelea kuwa pamoja mjengo huu huu,” alisema Spika
Ndugai akihitimisha nasaha zake.
No comments