KAULI YA SHIRIKA LA WANAWAKE BARANI AFRIKA KUFATIA KAULI YA RAIS MAGUFULI,WANAFUNZI WATAOPATA MIMBA WAKIWA SHULE
Matamshi ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu wanafunzi
wanaopata ujauzito kutoendelea na masomo yamezua gumzo kubwa na mijadala
mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Shirika la wanawake
barani Afrika limemtaka Rais Magufuli kuomba msamaha kutokana na matamshi yake
aliyoyatoa akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Pwani kuwa mwanafunzi
atakayepata ujauzito katika utawala wake hataweza kuendelea na masomo.
Hata hivyo, katika
sheria iliyopitishwa mwaka 2002 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu suala
la mtoto wa kike kupata ujauzito akiwa shule inaruhusu kufukuzwa shule na
kifungo cha miaka 30 kwa yule aliyesababisha ujauzito huo.
No comments