Breaking News

TRA YAFUNGA MADUKA YA WAFANYABIASHARA WASIOTUMIA MASHINE ZA EFD KARIAKOO


Afisa wa Kampuni ya Yono Auction Mart (kulia) na mmoja wa wafanya biashara wakifunga makofuli kwenye duka la madera katika mtaa wa Congo Kariakoo Dar es Salaam.


Wafanya biashara waliokamatwa eneo la Kariakoo Mtaa wa Congo Dar es Salaam, wakifunga maduka kufatia kukutwa na kosa la kutoitikia wito wa mamlaka hiyo kwenda kulipia faini kutokana na utoaji wa huduma pasipo kutoa risiti za kielektoniki licha ya kuwa na mashine wakifunga duka lao walipokamatwa na maofisa wa TRA.
 
Afisa wa Mamlaka ya Mapato Nchini (kushoto) akisubiri mmiliki wa duka la urembo lililokutwa likiendelea kufanya biashara hata baada ya kukutwa wakiuza bidhaa zao pasipo kutoa risiti za kielekroniki licha kuwa na machine inayotakiwa kutumika kwa utoaji wa risiti kwa wateja wao iliyotolewa na TRA.
 


Afisa wa Kampuni ya Yono Auction Mart akikagua moja ya duka la wafanyabiashara katika Mtaa wa Aggrey Kariakoo Dar es Salaam wakifanya biashara bila pasipo kutoa risiti ya kielektoniki licha ya kuwa na mashine hiyo. 
Afisa wa Kampuni ya Yono Auction Mart akifunga kofuli kwenye lango duka la wafanya biashara waliokamatwa katika Mtaa wa Aggrey Kariakoo Dar es Salaam wakifanya biashara bila pasipo kutoa risiti ya kielektoniki licha ya kuwa na mashine. 

Dar es salaam:
Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) imeendelea kufanya zoezi la ukaguzi wa maduka ya wafanya biashara wanaouza bidhaa zao pasipo kuwapatia risiti za mashine za Kielektroniki (Efd) jijini Dar es Salaam.

Kampeni hiyo imeendelea kufanyika katika eneo la Kibiashara la Kariakoo na itakuwa endelevu kuhakikisha wafanya biashara wanazingatia sheria, kanuni na taratibu za biashara katika mauzo ya bidhaa zao.

Afisa wa Kampuni ya Yono Auction Mart  ambao wanaendesha zoezi hilo kwa kushirikiana na jeshi la Polisi wakisimamia duka la mfanyabiashara waliokutwa wakiendelea kutoa huduma ilhali awali walikutwa wakiuza bidhaa hizo pasipo kutoa risiti ya kielektoniki licha ya kuwa na mashine.

Hatua ya ukamatwaji kwa wafanya biashara hao inatokana na kitendo cha kutokuitikia wito wa mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) wa kwenda kulipa faini baada kufanya kosa hilo.

Kwa kosa hilo watalazimika kulipa kati ya shilingi milioni 3 mpaka 4 na nusu ili waruhusiwe kuendelea na biashara.

(Picha zote na Robert Okanda Blogspot)





No comments