Breaking News

JITAHADA ZA RAIS DKT. SAMIA ZIMEKUZA SEKTA YA UTALII NCHINI - NAIBU WAZIRI KITANDULA

Naibu Waziri wa Maliasiri na Utalii Mhe. Dastan Kitandula akifafanua jambo mara baada ya ufunguzi wa onesho la 8 la kimataifa la Utalii la Kiswahili (S!TE 2024) katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Ephraim Mafuru akizungumzia dhumuni la kuandaa onesho la 8 la kimataifa la Utalii la Kiswahili (S!TE 2024) katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.

Frank Wandiba - Dar es salaam;
Naibu Waziri wa Maliasiri na Utalii Mhe. Dastan Kitandula amesema Sekta ya Utalii nchini imeemdelea kupiga hatua kubwa kutokana na jitihada zinazofanywa ana serikali ya wamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa kuweka Mazingira wezeshi katika Sekta hiyo.

Akizungumza mara baada ya akifungua jukwaa la uwekezaji katika sekta ya Utalii Nchini Tanzania katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam, ikiwa ni sehemu ya onesho la 8 la kimataifa la Utalii la Kiswahili (S!TE 2024).

Amesema kuwepo na Mazingira na sera nzuri za uwekezaji pamoja na miundombinu rafiki katika sekta hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kuwavutia watalii wengi kutoka mataifa mbalimbali kuja kuwekeza Nchini.

Alisema sekta ya Utalii nchini imekuwa no moja ya sekta inaingiza fedha nyingi za kigeni sambamba na kuchangia kiasi kikubwa katika pato la Taifa (DGP) hivyo Serikali itaendelea kuweka jitihada za msingi katika kuimarisha uwekezaji kwenye sekta hiyo.

"Sekta ya Utalii imekuwa ni moja ya sekta ambayo imekuwa ilizalisha ajira pamoja na inaingiza fedha za kigeni na kichangia kiasi kikubwa katika pato la Taifa, serikali inaendelea kuweka miundombinu mazuri kwa lengo la kuvitia uwekezaji katika Sekta ya hiyo".
Alisema Bw. Kitandula.

Kwa upande Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasi na Utalii Nkoba Mabula amesema serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuweka miundombinu wezeshi pamoja na kutunga sera ambazo zitasaidia kuvutia uwekezaji katika sekta ya utalii.

"Nitoe rai na kuwahimiza watu wote wanaohitaji kuwekeza wafike katika Ofisi za mamlaka za uwekezaji ikiwemo Kituo Cha uwekezaji Tanzania (TIC) na Kituo Cha uwekezaji serikali ya Mapinduzi Zanzibar (ZIPA) wapate taratibu hizo kuwekeza katika sekta hiyo". Alisema Bw. Mabula.
              
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Ephraim Mafuru onesho hilo ni kuwaleta pamoja watoa huduma wa Utalii Ndani na nje ya Nchi ambao watapata fursa ya kuonesha bidhaa zao za Utalii na kutengeneza Mtandao wa Biashara (Business Network), sambamba na Utekelezaji wa sera ya Taifa ya Utalii ya Mwaka 1999 pamoja na mkakati wa kutangaza Utalii Kimataifa ( 2020-2025 ) ambayo imetilia mkazo kutangaza Tanzania kama kivutio Bora cha Utalii Duniani.

No comments