Breaking News

SERIKALI ITOE ELIMU ZAIDI JUU YA FURSA ZILIZOPO UWEKEZAJI SEKTA HOTEL

Na Neema Mpaka:
Serikali imeshauriwa kujikita zaidi katika kuwajengea uelewa kwa wawekezaji wa sekta ya hotel nchini pamoja na kutangaza fursa zilizopo ili kuongeza wawekezaji wengi zaidi zaidi.

Ushauri huo limetolewa leo oktoba 12, 2024 jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Masoko wa Serena hotel, Ndugu Seraphin Lusala katika kongamano la jukwaa la kitaifa la wawekezaji kupitia utalii ambalo linafanyika sambamba na onesho la kiswahili international Tourism Expo (S!TE) katika ukumbi mliman city.

Alisema wawekezaji katika ya hotel nchini wanatakiwa kueleweshwa kuhusu fursa za uwekezaji Tanzania pamoja na kuwapa moyo kuwekeza ili kupunguza upungufu wa hotel jijini dare es salaam hasusani panapokuwa na wageni wengi kutoka nchi mbalimbali.

"Ili kupata wawekezaji wengi zaidi wa hotel ni lazima watambue faida za kuwekeza hivyo naishauri TTB na TIC kuwaalika wawekezaji kwa sababu Kuna fursa nyingi ambazo TIC inatoa zikifahamika ziitawapa hamasa zaidi kuja kuwekeza katika sekta hiyo ya hotel ". Alisema Bw. Lusala.

Alisema jiji kama la Dar es salaam likipata ugeni mkubwa kuanzia watu kama elfu tatu ama elfu nne Kuna kuwa hakuna vyumba vya watu kulala.

Katika hatua nyingine Ndugu Lusala ameongeza kuwa OKTOBA 26 wameandaa tamasha la Wine Festival lenye lengo la kuwaleta pamoja watengenezaji wine kutoka ndani na nje ya nchini kuwatanisha na wadau kutoka serikali pamoja na sekta binafsi.

Alisema katika Maonyesho hayo pia kutakuwa na mabalozi mbalimbali wanao wakilisha nchi zao lengo likiwa ni kuwaleta pamoja wazalishaji na wasambazaji hao kuonyesha bidhaa zao, kubadilishana mawazo na uzoefu juu ya bidhaa hiyo pamoja na kuwatafutia soko la Tanzania nchini na litakuwa likifanyika Kila baada ya miezi mitatu.

Ametaja Viingilio kuwa ni laki moja (Tsh 100,000) kwa mtu mmoja ambayo otamwezesha kula chakula pamoja na kinywaji chochote apendacho itaanza saa 9 Alasiri mpaka saa 5 usiku.

 

No comments