KAULI YA MHE SUMAYE KWA SERIKALI, AOMBA KUIVUMILIA CHADEMA
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye
amefunguka na kuitaka serikali ya awamu ya tano iwavumilie na itambue kuwa
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na viongozi wake ni chama
halali kinafanya kazi kama CCM inavyofanya kazi zake.
Sumaye aliyasema hayo jana baada ya
jeshi la polisi kuzuia msafara wao ambao ulikuwa na lengo la kutembelea na
kujionea utendaji kazi wa Manispaa ya Ubungo inayoongozwa na CHADEMA.
"Hili
si jambo la ajabu kwa sababu hata viongozi wa CCM kwa mfano hata Pole Pole
anazunguka halmshauri zote nchini, ila wanapozunguka wao hakuna tatizo ila
inapokuja viongozi wa CHADEMA kidogo tayari wanaanza mapambano, tunadhani huu
ni uonevu tu unaendelea wa kujaribu kuwafanya watu wengine wajisikie kwamba
hawana uhuru na nchi yao hili nafikiri si jambo jema.
"Serikali
tunaomba ituvumilie ijue kwamba CHADEMA pamoja na viongozi wake ni chama halali
kinafanya kazi kama CCM wanavyofanya kazi kwa hiyo mambo ya kuandamwa CHADEMA
kila mahali inatusikitisha sana" alisema Sumaye
Mbali na hilo Sumaye anasema vitendo
hivyo vinavyofanywa kwa viongozi wa CHADEMA ni kutaka kukatisha tamaa jitihada
zozote zinazofanywa na viongozi wa chama hicho hivyo anadai ni kitu ambacho
hakiwezi kuvumilika.
"Kwa
jambo hili mimi nataka tu kuimbia serikali kuwa hawatafanikiwa kwani wataleta
vurugu pasipo kuwa na sababu zozote zile, wawaache watu wafanye kazi zao hapa
hakuna siasa zozote tunazofanya.
"Tunakagua
miradi kwani halimashauri hizi ni zetu kama ambavyo wao wanatembea kwenye
halimashauri zote nchini kuona namna Ilani yao inavyotekelezwa na sisi tunataka
kujua viongozi wetu wa CHADEMA wanatekeleza vipi yale ambayo CHADEMA imewaagiza
kufanya katika Ilani yake. Na miradi hii ni kwa wananchi wote" alisisitiza Sumaye
No comments