WAZIRI SIMBACHAWENE AMTESEMA HAYA KUFATIA KAULI ALIYOITOA RAIS MAGUFULI KUWA ATAIFUTA HALMASHAURI KAMA MADIWANI WATALAZIMISHA KUMFUKUZA MKURUGENZI

Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Mh. George Simbachawene amefunguka na kutetea kauli ya
Rais magufuli aliyoitoa mkoani Kilimanjaro kuwa atafuta halmashauri hiyo kama
madiwani watadiliki kutaka kumtoa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ambaye yeye
amemteua.
Akitoa
ufafanuzi bungeni Simbachawene amesema kuwa Rais Magufuli alitoa kauli hiyo kwa
nia njema kwa kuwa wapo baadhi ya madiwani huwa wanataka kuwaondoa watendaji
hao kwa maslahi yao binafsi na kusisitiza kuwa ikitokea hivyo hata kabla ya
Rais hajachukua hatua ya kuvunja hiyo Halmashauri yeye ataanza kuivunja.
"Si
kweli kwamba kauli ya Rais Magufuli imeleta mkanganyiko, ile kauli Rais amemaanisha
pale unapokuwepo mkakati wa Madiwani kutaka kumuondoa Mkurugenzi wa
halimashauri kwa maslahi yao binafsi, haya yote huwa yanatokea .
"Rais
Magufuli hakusema kauli hiyo kuwalinda wabadhirifu bali pale unapokuwepo mpango
mkakati wa madiwani kwa wakurugenzi kwa chuki, ikitokea hivi mimi mwenyewe
nitaivunja hiyo halmshauri kabla hata Rais hajafanya maamuzi hayo" alisema
Simbachawene
No comments