CATHERINE RUGE ATEULIWA KUWA MBUNGE VITI MAALUM KUPITIA CHADEMA.
![]() |
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec)
imemteua Catherine Nyakao Ruge kuwa mbunge viti maalumu kupitia tiketi ya
Chadema.
Taarifa iliyotolewa ya Nec
imesema kuwa imemteua Ruge baada ya kukamilisha kikao ilichokifanya leo.
Katika taarifa hiyo Nec
imeeleza kuwa kikao hicho kilifanywa kwa mujibu wa Ibara ya 78(4) ya Katiba ya
Tanzania 1977 pamoja na Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,
Sura ya 343.
Uteuzi wa Ruge umefanyika baada
aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Dk Elly Macha kufariki dunia Machi 31, mwaka
huu.
|
No comments