SIMULIZI YA MZEE WA MIAKA 127, ANADAI ALIIONA VITA VYOTE VYA DUNIA NA MAJIMAJI VIKIPIGWA
WAKATI
Dunia ikiwa imeaminishwa kuwa binadamu aliyeishi miaka mingi alikuwa anatoka
nchini Italia na amefariki hivi karibuni, ameibuka mzee mmoja mkazi wa Kijiji
cha Majengo, Kata ya Ihanda Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya ambaye ana miaka 127.
Mzee
Ambilikile Mwanyaluke Panja, anaishi kitongoji cha Izyiga takribani kilomita
mbili kutoka Kituo cha Mabasi cha Ihanda upande wa Magharibi, na hajiwezi kwa
lolote kutokana na kuwa na umri mkubwa.
Kutokana
na umri wake kuwa mkubwa ambao umemfanya kushindwa kutembea, familia yake
inatumia kiti cha magurudumu kumsukuma wakati wa kumtoa nje na kumrudisha
ndani.
Anasema
Kabila lake ni Mndali na ni mzaliwa wa Kijiji cha Kapelekesi kilichopo katika
Kata ya Kafule wilayani Ileje na kwa mujibu wa maelezo yake alihamia Mbozi
baada ya vita ya kwanza ya dunia.
Baadhi
ya matukio ambayo mzee Panja anayakumbuka ni pamoja na Vita ya Majimaji ya
mwaka 1905 hadi 1907 ambayo anadai ilikuwa inapiganwa wakati yeye ana umri
mkubwa na anachunga ng’ombe kijijini kwao Kapelekezi.
Mzee
Panja anasema siri kubwa ya yeye kuishi miaka mingi ni aina ya vyakula
alivyokuwa anakula tangu akiwa mtoto mpaka hivyo karibuni alipoanza
kubadilishiwa.
Anasema
alikuwa anakula zaidi ugali wa dona na wa Ulezi, ndizi aina ya Matoki huku
mboga kuu ikiwa maziwa ya ng’ombe, maharage, Karanga na Njugu mawe.
Aidha
anasema kipindi hicho kulikuwa hakuna chumvi za kisasa na badala yake walikuwa
wanatumia chumvi za asili kwa kuchoma baadhi ya majani na kutumia majivu yake
kwenye mboga (Chipembekwa
No comments