HUU NDO UKWELI KUHUSU UNYWAJI WA SUPU YA PWEZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME
HAMU
ya tendo la ndoa kwa mwanadamu au mwanamke ni moja ya hisia za msingi kwa mtu
wa kawaida kama ilivyo njaa au usingizi.
Kwa
ajili ya matatizo mbalimbali yaliyo katika jumuiya, pamoja na kwamba tendo la ndoa
ni jambo la msingi kwa wale waliooana, kuna wanaume aidha hawana uwezo wa
kulifanya tendo hili au wana hisia ndogo na nguvu kidogo za kutekeleza tendo
hili.
Panapokuwa
na changamoto Fulani, wajasiriamali huiona changamoto hiyo kama fursa, na fursa
hiyo imeonekana kuwanufaisha vijana wanaokaanga samaki aina ya pweza katika
soko la samaki la kimataifa la magogoni baada ya supu ya samaki huyo aina ya
pweza kuonekana kupendelewa sana na wanaume wa rika zote nchini.
Lakini
siku za hivi karibuni hiki kitumbua kimonekana kuingia mchanga, yaani biashara
kuharibika baada ya uvumi kwenye mitandao ya kijamii kudai kwamba wakaanga
samaki wanaweka dawa za kuongeza nguvu za kiume aina ya viangra ili kuisisimua
miili ya wateja wao, mwandishi wetu Austin Beyadi amezungumza na baadhi ya
wakaanga pweza katika soko la samaki ili kupata ukweli kuhusu tuhuma hizo.
Mwenyekiti
wa ukanda wa wakaanga samaki amesema hakuna ukweli wowote wa wakaanga
samaki kuweka madawa ya kuongeza nguvu bali vinaweka viungo vya kawaida kama
anavyofafanua.
Ni
imani ya wanaume wengi wa pwani na hata kutoka bara ambao huishi ukanda wa
pwani siku hizi hupenda supu ya pweza kutokana na wingi wake wa virutubisho
ambavyo huamini kuwa vinaongeza nguvu za kiume kwa waliopungukiwa.
Baadhi
ya vijana waliozungumza na Clouds Tv wamedai kwamba mara nyingi wanatumia supu
ya pweza ili kusisimua mwili huku wengine wakidai wanatumia kama kiburudishotu
sio kama dawa ya kuongeza nguvu.
ULAJI
wa supu ya pweza, kwa dai kwamba vinaongeza urijali kwa wanaume kumeelezwa kuwa
ni dhana potofu inayostahili kupigwa vita kwa kuwa haina uhusiano kati ya
urijali wa mwanaume na virutubisho vinavyotolewa na chakula hicho.
Kwa
siku za hivi karibuni vijana wengi wameonekana kuchangamkia matumizi ya dawa za
kuongeza nguvu za kiume bila kushauriwa na daktari, ANNA …… ni mfanyabiashara
wa duka la dawa na hapa anaeleza wateja wake ni akina nani.
No comments