MHE LOWASSA AMESEMA HAYA MARA BAADA YA KUTOKEA AJALI YA BASI LA WANAFUNZI KARATU.

Waziri
mkuu mstaafu, edward lowassa ametuma salamu za rambi rambi kutokana na tukio la
watu 32 kufariki dunia katika ajali ya basi.
Waliofariki
katika ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi karatu, ni wanafunzi 29, walimu
wawili, pamoja na dereva wa gari hilo.
“nimepokea
kwa masikitiko taarifa ya ajali hiyo, ni ajali mbaya ambayo inaifanya siku hii
kuwa mbaya katika historia ya nchi yetu,”alisema
Miongoni
mwa wanafunzi waliofariki ni pamoja na wanaume 11 na wasichana 18.
Kadhalika
maiti 32 zikiwamo za walimu wawili, dereva mmoja na wanafunzi 29 zimepokelewa
sasa hivi katika hospitali ya lutheran karatu.
No comments