MASOUD KIPANYA: HAKUNA MWANAUME ANAYERIDHIKA NA MWANAMKE MMOJA. UKIONA KATULIA NA MMOJA BASI ANA MATATIZO AU UCHUMI UMEKAA VIBAYA

Mtangazaji
na Mchoraji katuni maarufu nchini Tanzania,Masoud Kipanya amewaaacha watanzania
midomo wazi kwa kuweka wazi maoni yake kuwa mwanaume hawezi kuridhika na
mwanamke mmoja.
Masoud
amesema tangia zamani wanaume ni Watu mwenye tamaa hivyo hakuna mwanaume ambae
anapenda kuwa na mwanamke mmoja ila ni vitu vidogo vidogo tu vinavyozuia kama
dini ya Kikristo na masuala mengine ya kiuchumi.
“Hakuna
mwanaume anaependa kuwa na mwanamke mmoja,na hiyo ndiyo huruka ya
uanaume,tunajizuia tu kwa sababu!! hivyo kwa mfano kwa wenzangu wakristo
utaratibu unawazuia lakini angalia vidumu vilivyo nje unaona eeehh??“Amesema
Masoud Kipanya kwenye Mahojiano yake na Kwanza TV.
Hata
hivyo Masoud alizungumzia suala la idadi ya kuzaa watoto kwenye familia na
kusema kuwa kwa upande wake yeye hana
kikomo kwenye kuzaa kwani anaamini watoto hawarishwi na yeye bali wanarishwa na
mwenyezi Mungu.
Masoud
Kipanya kwa mujibu wa Takwimu za mwaka jana zilizofanywa na kituo cha Clouds FM
kupitia kipindi cha XXl ni moja ya watu watatu maarufu nchini Tanzania
wanaoendesha magari ya kifahari akiwa anamiliki gari aina ya Hummer H3.
==>Msikilize
hapo chini akiongea
No comments