HUYU NDIYE MBUNGE ALIYEMWAGA CHOZI AKICHANGIA BUNGENI KUHUSU UDHALILISHWAJI WA WATOTO

Mbunge
wa Viti Maalumu (CCM) Faida Bakari amemwaga chozi bungeni akielezea
udhalilishaji unaofanywa kwa watoto nchini.
Faida
akichangia bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto kwa mwaka wa fedha 2017/18 bungeni jana mjini Dodoma alisema watoto
wanadhalilishwa kwa kufanyiwa vitendo vibaya na watu wazima. Aliiomba Serikali
kuchukua hatua kali dhidi ya wanaobainika kufanya hivyo.
“Watoto
wanaharibiwa mheshimiwa waziri, naomba mchukue hatua kali za kisheria kwa watu
hawa. Nilienda Pemba nililia watoto wanaharibiwa maumbo. Mheshimiwa nasema kwa
uchungu,” alisema huku akilia na kuvuta pumzi ndefu kabla ya kuendelea
kuzungumza.
Alisema
walimu wamekuwa wakiwadhalilisha watoto huko Pemba na kumuomba waziri
ashughulikie suala hilo.
“Tumrudie
Mungu, unakuta mibaba mizima inawapa mimba watoto na madevu yao mengi wanawatia
watoto wenzao mimba,” alisema.
Faida
pia alisema wazee wamekuwa wakinyanyaswa katika jamii na kuwataka Watanzania
kuwatunza kwa sababu ipo siku nao watakuwa wazee. “Ukiona nyumba zao unalia
naomba mheshimiwa uangalie katika eneo
hili la wazee.”
Mbunge
wa Viti Maalum (Chadema), Suzan Lyimo yeye alisema wazee wametelekezwa katika
kambi za kuwahudumia na kuitaka Serikali kuwaangalia.
“Mwaka
jana mlisema mtaleta Sheria ya Wazee lakini mwaka huu haikuzungumzwa, hakuna
sheria ya wazazi ndiyo maana wazee bado wanauawa,” alisema.
No comments