HALOTEL YATOLEA UFAFANUZI JUU YA KUTOKUHUSIKA NA MAKOSA YA UHUJUMU UCHUMI
Mkurungenzi
mtendaji wa halotel Tanzania bw. Le Van Dai akitoa ufafanuzi katika mkutano na
waandishi wa habari (hawapo) mapema leo jijini Dar es salaam.
Mwanasheria
wa kampuni ya Viette Tanzania LTD (Halotel), Bw Christopher Masai akifafanua
jambo katika mkutano wa waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar
es salaam.
Mwanasheria
wa kampuni ya Viette Tanzania LTD (Halotel), Bi Fatma Seif akizungumza katika
mkutano wa waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar es salaam
Dar es Salaam
Kampuni
ya mawasiliano ya simu ya Halotel imetoa ufafanuzi kuhusu tuhuma zilizokuwa zikihihusha kampuni hiyo ya kuisababishia
serikali hasara ya shilingi milioni 459 ambapo wao wamehusishwa
na vipengele viwili vya mashtaka.
Mashtaka
hayo ya Halotel ni kushindwa kutoa taarifa ya usajili wa kampuni ya mitambo ya UNEX Limited
ambayo haikuwa kampuni iliyosajiliwa kikamilifu na TCRA kwaajili ya kusajili line za simu 1000
zilizouzwa kwa kampuni hiyo pamoja na kushindwa kutimiza majukumu yao
vizuri ya kuuza line za simu 1000.
Akizungumza
mapema leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Halotel Tanzania Bw. Le Van Dai amefafanua juu ya kutokuhusika na makosa ambayo yaliwahusisha watuhumiwa
wengine ambao ni wateja wa kampuni hiyo
ikiwa ni pamoja na usimikwaji wa mitambo hiyo.
Alisema
kuwa kampuni hiyo imekuwa ikiendesha ikiendesha shughuli zake nchini kwa kufata sheria na taratibu zote za mawasiliano ambazo zinatambuliwa na mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA).
Bw
lai aliongeza kuwa kwa mujibu wa mashtaka
yaliyosainiwa na mwendesha mashtaka mkuu wa serikali kuwa Mei 16 mwaka huu ambayo yanayoitaja kampuni
hiyo kuhusika na makosa hayo.
Alisema
mujibu kifungu namba 6 na 7 ambavyo havihusishi kampuni hiyo na makosa ya
washtakiwa wengine ambao sio wafanyakazi wa kampuni hiyo na kuongeza kuwa
hawana ushirikiano wowote na kampuni hiyo pamoja na raia hao wa
Pakistani zaidi ya kuiuzia laini za simu kampuni hiyo baada ya kuwasilisha
nyaraka zisizo halali.
“Sisi kama kampuni tunafanya kazi kwa usajili na
vibali halali vya mamlaka husika nchini
na tumekuwa wawazi na kufata vibali kutoka mamlaka husika pamoja na kufata
taratibu zote za kisheria " alisisitiza
Dai
No comments