Breaking News

IITA YAWANOA WANAFUNZI WAPENDE MASOMO YA SAYANSI

 Mkurungenzi wa Taasisi ya kimataifa ya utafiti wa kilimo cha kitropiki Tanzania (IITA) Dkt Victor Manyong akiongelea maadhimisho ya siku ya kilimo duniani ambapo nchini imeadhimishwa kwa kuwakutanisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali kuwajengea hali ya kupenda masomo ya sayansi mapema leo jijini Dar es salaam.
Mkuu wa kitendo cha mawasiliano wa Taasisi ya kimataifa ya utafiti wa kilimo cha kitropiki Tanzania (IITA),Bi, Catherine Njuguna akitoa ufafanuzi kuhusu maadhimisho ya siku ya kilimo duniani mapema leo jijini Dar es salaam


Mmoja ya watafiti wa Taasisi ya kimataifa ya utafiti wa kilimo cha kitropiki Tanzania (IITA) akitoa maelekezo jinsi taasisi hiyo inavyoendesha shughuli zake za kiutafiti kwa wanafunzi kutoka shule mbalimbali mapema leo Jijini Dare s salaam.

Dar es Salaam
Taasisi ya kimataifa ya utafiti wa kilimo cha kitropiki (IITA) leo imeadhimisha siku ya umuhimu wa mimea duniani kwa kusherehekea na watoto wa shule ili waweze kujifunza masomo ya kisayansi kwa  bidii.

Akizungumza katika maadhimisho hayo mkurugenzi mtendaji taasisi ya kimataifa ya utafiti wa ya kilimo cha kitropika (IITA),  Bw.Victor Manyong alisema taasisi hiyo imekuwa ikijishughulisha  na utafiti wa kilimo ili kuwasaidia wakulima katika mchakato wa kilimo na ndiyo mana siku hii hushirikisha watoto ambao ni vema wakipata mafunzo tangu awali ili kufikia mafanikio ya kisayansi.

Mkurugenzi Manyong amesema kuwa changamoto mbalimbali zimekuwa zikiwakabili wakulima kwa kukosa vitendea kazi vya kisasa pamoja na upungufu wa pembejeo na mbegu.

kwa upande wake afisa mawasiliano wa Taasisi hiyo Bi Catherine Njuguna alisema matokeo ya tafiti zao ambazo wamekuwa wakifanya sehemu mbalimbali nchini wamegundua kuwepo na changamoto nyingi sana hususani magonjwa ya mimea.

alisema pamoja na wataalamu kushauri juu ya njia bora za kutumia kwa wakulima hususani wadogo bado kumekuwepo na mwamko mdogo kwao hususani katika swala la matumizi sahihi ya pembejeo pamoja na ushauri wa wataalam wa kilimo.

Maadhimisho ya siku ya umuhimu wa mimea duniani huadhimishwa tarehe 14 mwezi mei.

No comments