JAMBAZI WA KIKE AUAWA JIJINI NAIROBI KENYA
Pichani
ni mwanamke ambaye ni jambazi anaejitambulisha kama mwanafunzi wa chuo kikuu
Mwanamke
anayedaiwa kuwa jambazi sugu, ambaye amekuwa akipakia mtandaoni picha zake
akiwa amejipodoa na kujipamba, ameuawa na polisi jijini Nairobi nchini Kenya.
Kijana
huyo ambaye ametambuliwa kama Claire Mwaniki aliuawa na polisi alfajiri na
mapema Jumatano katika mtaa wa kayole.
Gazeti
la kibinafsi la Daily Nation linasema mwanamke huyo alikuwa na majambazi
wengine wanne wa kiume pale walipofumaniwa na polisi wakitekeleza wizi katika
eneo la Lower Chokaa, mtaa wa Kayole.
Anadaiwa
kufyatulia risasi maafisa wa polisi akiwa na jambazi mwingine lakini wawili hao
wakauawa.
Wenzake wafanikiwa kutoroka.
Taarifa
katika gazeti la Daily Nation inasema polisi waliwaandama baada ya kupokea
taarifa kutoka kwa wenzao kupitia WhatsApp kwamba majambazi hao walikuwa
wamekwepa mtego waliokuwa wamewekewa.
Polisi
walijiandaa na kisha wakawakabili katika mtaa wa Lower Chokaa.
Mkuu
wa polisi wa mtaa wa Kayole Joseph Gichangi amenukuliwa na gazeti la Daily
Nation akisema: "Kwa mujibu wa wadokezi wetu, mwanamke huyo alikuwa mke wa
mshukiwa wa ujambazi ambaye anafahamika vyema, ambaye bado anasakwa na
polisi."
Alisema
visa vya wanawake kujihusisha na magenge yanayotekeleza wizi wa kutumia mabavu
vinaongezeka.
Wakenya
mtandaoni wamekuwa wakisambaza picha za Mwaniki na kumjadili sana mtandaoni.
Katika
Facebook, mwanamke huyo anajitambulisha kama mwanafunzi wa zamani wa chuo kikuu
cha Nairobi na mtu anayependa kufurahia maisha.
Kuna
wakati alipakia picha yake, ya mwanamume na mtoto, na kuongeza kwamba hiyo ni
"familia".
Mkuu
wa polisi Nairobi Japheth Koome anasema magenge mengi ya wahalifu huwa na
wanawake.
"Wanawake
hutumiwa kusafirisha silaha, kukusanya habari na hata kushiriki katika
ujambazi," Bw Koome alisema.
Aliongeza
kuwa wakati mwingine hutumiwa na majambazi wa kiume kuwapelekea chakula
mafichoni.
Chanzo-BBC
No comments